• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 5:20 PM
Kenya yashinda riadha za Afrika Mashariki nchini Tanzania

Kenya yashinda riadha za Afrika Mashariki nchini Tanzania

Na GEOFFREY ANENE

KENYA iliibuka mshindi wa Riadha za Afrika Mashariki za chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18 na 20 ugani Benjamin Mkapa mjini Dar es Salaam, Tanzania, mnamo Jumamosi.

Ilizoa dhahabu tisa katika siku ya mwisho ya mashindano hayo ya siku mbili kupitia kwa Duncan Kipng’eno (200m U20), Evans Kipkosgei (5,000m U18), Penina Mutisya (200m U20), Judy Kemunto, Diana Khisa na Evaline Chepkoech (4×400m U20), Christine Musembi (kurusha mkuki U18), Brian Muange (1,500m U18), Jensine Ligoo (kuruka umbali U18), Diana Cherotich (5,000m U20) na Samuel Toili, Brian Kiptum, Justus Muasya na Sabastian Kakaya (4x400m U20).

Katika siku ya kwanza, Kenya ilipata dhahabu kupitia kwa Jackline Nguyen (100m U18), Justus Muasya (5000m U20), Dorcas Chepkemoi (800m U18), Kelvin Koech (800m U18), Brian Kiptum (800m U20), Kemunto (400m U20), Nancy Cherop (3,000m U18), Beatrice Machoka (400m U18), Sebastian Simoti (400m U20), Irene Jepkemboi (kurusha mkuki U20) na Toili, Kelvin Koech, Brian Muange na Amos Kipkemboi (4x400m kupokezana vijiti).

Waliovunia Kenya nishani za fedha ni Diana Khisa (200m U20), Brian Muange (5,000m U18), Marion Chepng’etich (5,000m U20), Sharon Moraa (100m U18), Amos Kipkemoi (800m U18), Nicholas Kipng’etich (kuruka umbali U20), Sammy Kiplagat (800m U20) na Mercy Bosibori (400m U18). Mercy Chepkemoi (5,000m U20).

Wanariadha kutoka Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Zanzibar, Sudan Kusini, Eritrea na Burundi walishiriki makala ya mwaka huu.

Mabingwa wa 2022 Ethiopia hawakushiriki. Kenya ilimaliza makala yaliyopita katika nafasi ya pili kumaanisha wamepiga hatua kubwa mwaka huu.

  • Tags

You can share this post!

Ashtakiwa kwa kumchoma ‘ex’ kwa maji moto

Shehena ya kwanza ya mahindi ya manjano kutua leo Jumapili

T L