• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Asukumwa jela miaka mitano kwa kudai pesa za fidia za mtu aliye hai

Asukumwa jela miaka mitano kwa kudai pesa za fidia za mtu aliye hai

Na RICHARD MUNGUTI

MLAGHAI alifungwa Jumatano miaka mitano na miezi minne gerezani kwa kughushi hati ya kifo cha binamuye na kujaribu kuibia kampuni ya Bima ya Britam Sh500,000.

Solomon Kithuka Kyalo alisukumwa jela na hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bw Bernard Ochoi alipokiri alighushi cheti cha kifo cha Mutisya Musyoki aliyekuwa ameweka bima na Britam.

Bw Ochoi alisema mshtakiwa alitumia uwongo kujaribu kufaidi kwa kujipatia pesa kwa njia ya undanganyifu. “Bw Musyoki yuko hai, hajakufa,” hakimu alielezwa na kiongozi wa mashtaka.

Kyalo, hakimu alielezwa alikamatwa mapema mwaka huu akijaribu kuibia Benki ya Faulu Sh250,000 akitumia cheti hicho hicho cha kifo cha Bw Musyoka. Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda alieleza hakimu kuwa mshtakiwa yuko na mazoea ya kulaghai benki na kampuni za bima akitumia ujanja.

“Naomba hii mahakama imchukulie hatua kali mshtakiwa kwa vile amekuwa na mazoea ya kulaghai kampuni za bima na benki ,” Bw Gikunda alimweleza hakimu, Mahakama ilielezwa mshtakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza.

Akijitetea mshtakiwa aliomba msamahama akisema ni ushawishi mbaya unaomsukumu kutenda uhalifu. “Nimejifunza kwa njia ngumu kwamba uhalifu haulipi. Naomba mahakama inisamehe,” mshtakiwa alimsihi hakimu huku akimweleza ameghairi makosa yake.

Akipitisha hukumu , Bw Ochoi alimweleza mshtakiwa kwamba kudanganya kwamba mtu ameaga ili ulaghai ni makosa mabaya. Bw Ochoi alimweleza mshtakiwa ijapokuwa ameokolea mahakama muda kwa kukiri mashtaka , hiyo siyo sababu ya kutoadhibiwa vikali.

Bw ochoi alimfunga jela miaka mitano na miezi minne. Mshtakiwa alikiri mnamo Machi 17 2021 alighushi cheti cha kifo cha Bw Musyoki

 

 

  • Tags

You can share this post!

Babu wa miaka 75 kusalia rumande

FAUSTINE NGILA: Safaricom ikomeshe teknolojia ya kidole kwa...

T L