• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 12:41 PM
Babu wa miaka 75 kusalia rumande

Babu wa miaka 75 kusalia rumande

Na RICHARD MUNGUTI

MZEE mwenye umri wa miaka 75 aliyekuwa ametoroka mahakama katika kesi ya wizi wa Sh2.4milioni atakaa rumande hadi Oktoba 27,2021.

Waweru Gicho Waweru alikuwa anasakwa na maafisa wa polisi waliokuwa wameagizwa na Mahakama za Milimani , Embu na Kibera atiwe nguvuni. Waweru alikuwa ametolewa cheti cha kumkamata baada ya kukwepa kufika kortini wakati wa kusikizwa kwa kesi zinazomkabili.

Mshtakiwa anayekabiliwa na msururu wa kesi alijitetea kupitia kwa wakili wake kwamba amekuwa mgonjwa wakati huu wote alipokuwa akisakwa na mahakama.

“Niko na ripoti za hospitali kuonyesha nilikuwa mgonjwa na wala sikuwa nimetoroka kesi,” mshtakiwa alimweleza hakimu. Mahakama ilifahamishwa “mshtakiwa yuko tayari kufikishwa kortini Alhamisi kwa maagizo zaidi katika kesi hizo nyingine.”

Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana kwa “ kadhaa kudhirisha” Lakini kiongozi wa mashtaka Anderson Gikunda alieleza mahakama kwamba mshtakiwa anasakwa na mahakama za Embu na Nairobi.

Hakimu alielezwa ajuza huyo alikamatwa Jumanne na kuzuiliwa. Mahakama  iliombwa isimwachilie mshtakiwa kwanza akamilishe kesi na mahakama hizo za Embu , Kibera na Milimani kabla ya kuachiliwa kwa dhamana.

Shtaka la kwanza dhidi ya mshtakiwa ni kuwa mnamo Septemba 2017 aliibia benki ya Kenya Commercial Bank tawi la Wastegate. Amekana aliiba Sh2.4milioni na kujaribu kuchomoa Sh1.2milioni kabla ya kukamatwa.

Hakimu alikataa kumwachilia kwa dhamana mshtakiwa hadi mahakama nyingine zikamilishe kesi dhidi yake.

  • Tags

You can share this post!

Shinikizo DPP Noordin Haji ang’atuke yapelekewa PSC

Asukumwa jela miaka mitano kwa kudai pesa za fidia za mtu...

T L