• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 10:48 AM
Asukumwa jela miaka miwili kwa kupatikana na pingu

Asukumwa jela miaka miwili kwa kupatikana na pingu

Na RICHARD MUNGUTI

AFISA wa kijeshi (KDF) aliyetimuliwa kazini atatumikia kifungo alipokiri shtaka la kujitambulisha kuwa afisa wa Polisi.

Joseph Rotich aliyefungwa na hakimu mwandamizi Bw Peter Mutua alipatikana akiwa na pingu, mali ya idara ya Polisi.Kabla ya kusukumwa jela miaka miwili, Rotich alikuwa amekamilisha kifungo cha mwezi mmoja gerezani kwa kujitambua kuwa afisa wa polisi.

Mshtakiwa alikabiliwa na shtaka la kujitambulisha kwa maafisa wawili wa polisi kwamba ameajiriwa na idara ya polisi katika mtaa wa Kawangware.Alikiri shtaka la kupatikana na mali ya serikali.

Vifaa vya serikali ambavyo mmoja anaweza kujikuta amenaswa na serikali akiwa nazo ni yunifomu ya maafisa wa usalama , pingu , jaketi, kirauni na pingu.Rotich alikiri alipatikana na pingu akiwa na nia ya kuzitumia vibaya.

Alijitambua kwa maafisa wa polisi katika kituo cha Polisi cha Muthangari kwamba ameajiriwa na huduma ya polisi.Hakuwa na kitambulisho cha kuonyesha ameajiriwa na idara hiyo ya polisi.Mshtakiwa alipewa siku 14 kukata rufaa kama hakuridhika na adhabu ya kulipa faini ya Sh200,000 ama atumikie kifungo cha miaka miwili.

Alipohukumiwa mwezi mmoja mshtakiwa alikuwa ametozwa faini ya Sh50,000 lakini akashindwa kuilipa.

 

  • Tags

You can share this post!

Yaya afungwa miaka miwili kwa kuiba mikufu

Waliompora mwanafunzi washtakiwa