• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Atokwa jasho jingi viganja vya miguu

Atokwa jasho jingi viganja vya miguu

Na MWANDISHI WETU

Mpendwa Daktari,­­­Mwanangu mvulana ambaye ametimu umri wa kubalehe ana tatizo la kutokwa na jasho kwenye viganja na miguu yake.

Shida hii ilianza miaka kadha iliyopita na sijaweza kupata suluhu la kudumu. Kuna nyakati ambapo nyayo vile vile viganja vyake huanza kuonyesha nyufa na kumkosesha starehe. Tutakabilianaje na tatizo hili?Irene, Mombasa Mpendwa Irene,Kutokwa na jasho ni mojawapo ya mbinu za kudhibiti joto jingi mwilini.

Mtu anapotokwa na jasho kupindukia kiasi cha kumkosesha utulivu, sawa na tatizo linalomkumba mwanao, hali hii inafahamika kama hyperhidrosis. Kutokwa na jasho kupindukia sio hatari. Kulowa kila mara kwa viganja na miguu kunatoa mazingira mwafaka kwa matatizo ya ngozi kama vile maambukizi ya kuvu, ukurutu(eczema) na hata nyufa.

Mara nyingi kutokwa na jasho kupindukia huwa kunatokana na shughuli nyingi kwenye tezi za jasho, hali inayoletwa na upungufu wa mawasiliano kutoka kwa neva.Miongoni mwa watu wachache, huenda kukawa na matatizo mengine ya kiafya kama vile matatizo ya homoni, sukari kwenye damu na wasiwasi mwingi.

Mwanao anapaswa kunywa maji mengi na pia anapaswa kuwazia kuvalia nguo zisizombana, soksi zilizoundwa kwa kitambaa cha pamba na viatu vilivyoundwa kwa ngozi ya ng’ombe.Anaweza badilisha soksi na viatu katikati ya siku ikiwa itawezekana, na kuvalia viatu wazi wakati wa jioni.

Pia, anaweza jipaka dawa ya aluminium chloride/chlorhydrate kuambatana na ushauri wa daktari au mwanafamasia. Krimu ya kudumisha unyevu (moisturising cream) pia yaweza saidia kukabiliana na nyufa kwenye nyayo na viganja.

Ikiwa atazidi kutokwa na jasho kupindukia, basi litakuwa jambo la busara iwapo atakaguliwa na daktari wa ngozi kubaini ikiwa anakumbwa na iontophoresis, hali inayomaanisha kwamba mkondo wa umeme unapitishwa hadi kwa miguu na mikono kupitia maji.Mpendwa Daktari,Nilikuwa nikitokwa na maji maji ukeni wakati wa ujauzito.

Nilitibiwa lakini tatizo hilo limerejea baada ya kujifungua mapema mwaka huu. Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa maabara, daktari aliniambia kwamba hali hii hutokea sana wakati wa ujauzito. Kwa nini inanikumba tena?Jackie, NairobiMpendwa Jackie,Mara kwa mara wanawake hukumbwa na tatizo la kutokwa na majimaji ukeni.

Wakati mwingi, tatizo hili hutokana na maambukizi ya bakteria au ukuvu kutokana na kutokuwa na usawa wa viumbehai wanaoishi katika sehemu hii ya mwili. Ikiwa viumbehai hawa watapungua, kwa mfano bakteria nzuri, basi viumbehai hao wengine hujizidisha kwa idadi na kusababisha kuvuja kwa majimaji kusiko kawaida, mwasho na hata wakati mwingine uchungu.

Hali hii hasa hutokea wakati wa ujauzito kutokana na mabadiliko ya kihomoni, lakini pia yaweza wakumba wanawake ambao sio wajawazito, au hata wasichana.Tiba huwa rahisi na thabiti huku mgonjwa akitarajiwa kutumia tembe za kumeza au za kuingizwa ukeni.

Ili kuzuia maambukizi, valia suruali za ndani zilizoundwa kwa kitambaa cha pamba na usivalie long’i zinazokubana.Ikiwa mpenzi wako anaonyesha ishara zozote, anapaswa kutibiwa japo maambukizi ya kutokwa na majimaji ukeni hayasambazwi kupitia tendo la ndoa.

  • Tags

You can share this post!

Corona hatari sana yaja hata kwa waliopata chanjo –...

Siasa ndizo mwiba kwa Mumias Sugar