• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 2:00 PM
Shinikizo DPP Noordin Haji ang’atuke yapelekewa PSC

Shinikizo DPP Noordin Haji ang’atuke yapelekewa PSC

Na RICHARD MUNGUTI

HOJA ya kumtimua kazini mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) Noordin Haji iliwasilishwa na mawakili zaidi ya 10 kwa tume ya kuajiri watumishi wa umma (PSC).

Wakiongozwa na mawakili  Danstan Omari , Cliff Ombeta , Bi Swiga Matina na Paul Macharia wanasheria hawa wanadai Bw Haji amezembea kazini. Omari alisema hoja ya Rais Kenyatta kuafikia ahadi zake zinatakwamishwa na jinsi DPP atakavyotekeleza majukumu yake.

“Asilimia 60 ya pesa alizopelekewa na maafisa kutoka idara ya uchunguzi wa jinai kwa ushauri hajazisoma na kuzihidhinisha kama anavyotakiwa,” mawakili hao walilalamika.

Wanasheria hao walimtaka Bw Haji ajihuzulu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake. Bw Omari alimshauri Bw Haji ang’atuke kabla ya kutimuliwa kwa umma. “Namsihi ang’atuke  pasi kusukumwa na umma,” Bw Omari .

Wakiwahutubia wanahabari katika mahakama kuu ya Milimani mawakili hao wamedai , DPP amekuwa akiwabagua washukiwa anaopendekeza wakamatwe na kushtakiwa.

Wakili Paul Macharia aomba hatua ichukuliwe dhidiya DPP noordin Haji….Picha/RICHARD MUNGUTI

Bw Omari alimkosoa Bw Haji kwa kuamuru Inspekta Jenerali wa Polisi amchunguze afisa mmoja mkuu wa polisi kutoka kitengo cha DCI aliyechunguza kesi ya mauaji ya raia wa Uholanzi Tob Cohen.

“Ikiwa DPP anaagiza mchunguzi huyo achunguzwe kwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kumpendekezea wanaopasa kukamatwa na kushtakiwa basi haki iko wapi,” alihoji Bw Omari.

Wakili huyo alihoji nia ya DPP kuamuru kesi dhidi ya mshukiwa kufungwa bila mashtaka ilhali uchunguzi wa DCI ulimlenga barabara. Mawakili hao walipeleka ombi lao kwa PSC iliyomwajiri DPP iizikize na kumtimua kazi kiongozi huyu wa mashtaka. Bw Omari amesema kuwa ombi DPP ang’atuliwe liko na mashiko kisheria na linatega hisia za umma.

Katika ombi hilo walalamishi hao wameambatanisha msururu wa kesi wanazodai Bw Haji ameshindwa kutoa mwelekeo. Bi Swiga Matina amemkosoa DPP kwa kuzembea kazini akisema “huenda uhusiano wa nchi hii na mataifa ya kigeni ukazorota.”

Bw Ombeta alishangaa sababu DPP hawezi kuchukua hatua ikitiliwa maanani hawezi pata maagizo jinsi anavyotekeleza majukumu yake. Mawakili hao walidai wakati umewadia “upendeleo kuhusu wanaotakiwa kushtakiwa upigwe teke na wahusika wakuu wote washtakiwe.”

 

 

  • Tags

You can share this post!

Kijana anayelenga kutinga upeo wa kimataifa miaka ijayo

Babu wa miaka 75 kusalia rumande

T L