• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Baunsa taabani kwa kumjeruhi mteja klabuni

Baunsa taabani kwa kumjeruhi mteja klabuni

NA TITUS OMINDE

‘BAUNSA’ mmoja kutoka klabu maarufu mjini Eldoret iliyoko kando ya barabara ya Eldoret-Kapsabet ameshtakiwa kwa kumpiga mteja katika klabu hiyo na kumjeruhi vibaya mwilini.

Amos Tekis mwenye umri wa miaka 35 almaarufu Sendee anadaiwa kumjeruhi daktari wa Eldoret katika klabu ya Tamasha.

Hati ya mashtaka ilisema kuwa kisa hicho kilitokea katika kilabu ya Tamasha katika Kaunti Ndogo ya Kapseret usiku wa Novemba 27, 2022.

Mahakama iliambiwa kwamba mshtakiwa alimvamia Dkt Evans Rono na kumsababishia madhara makubwa kinyume na kifungu cha 234 cha kanuni ya adhabu.

Polisi wamekuwa wakichunguza tukio hilo tangu liliporipotiwa katika kituo cha polisi cha Langas mnamo Novemba 28, 2022.

Mlalamishi alirekodi taarifa baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali moja mjini humo na kujaza fomu ya P3.

Bw Tekis ambaye Jumatano alifika mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi Peter Areri, alikanusha shtaka hilo na kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Sh10, 000.

Tayari mwajiri wake alimfuta kazi baada ya tukio hilo.

Kesi hiyo itasikilizwa Julai 6.

Tukio hilo ni moja ya matukio mengi ambapo wapiga mabaunsa huwavamia wateja katika sehemu mbalimbali za burudani wakichukua sheria mkononi.

Baadhi wateja husika kutoka Eldoret wameelezea wasiwasi wao kutokana na ongezeko la visa vya mabaunsa kuwashambulia mara kwa mara bila kufuata sheria.

“Hawa watu wanajifanya kama wanatumia sheria zao. Wengi wao hawana adabu kwa wateja wao. Kuna visa vingi vya ukatili dhidi ya watu wanaojivinjari katika mji huu, nyingi ya kesi hizi haziripotiwi,” Elijah Ayieko, wakili Eldoret alisema.

Bw Ayieko aliwaonya wapiga debe dhidi ya kuchukua sheria mkononi mwao.

Wakili huyo alisema kutokana na imani nyingi potovu kuhusu kile ambacho mabaunsa wanaruhusiwa kufanya, wengi wanateswa kutokana na ukatili wa mabaunsa.

Mnamo 2019 mwanamume mmoja ambaye alipigwa na baunsa katika Klabu ya Eldoret alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Moi.

Sera kuhusu jukumu la baunsa inasema kwamba hawako huru kushiriki kutumia nguvu au vurugu kupita kiasi wanavyoona inafaa.

Hata hivyo, wanaweza kutumia nguvu tu ikiwa itatumiwa dhidi yao kwanza kama haki za raia yeyote wa kawaida kujilinda dhidi ya uvamizi.

Katika hali nyingi wapiga mabaunsa hufunzwa kurekebisha hali kupitia mawasiliano badala ya nguvu za kimwili.

 

  • Tags

You can share this post!

Faith Chepng’etich amezea mate 42km baada ya Sifan...

Ashtakiwa kwa kujifanya ‘chokoraa’ akiuza chang’aa

T L