• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:44 PM
Faith Chepng’etich amezea mate 42km baada ya Sifan kutawala London Marathon

Faith Chepng’etich amezea mate 42km baada ya Sifan kutawala London Marathon

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Ligi ya Almasi, Jumuiya ya Madola, dunia na Olimpiki mbio za mita 1,500, Faith Chepng’etich amepata motisha kubwa ya kujitosa katika marathon kutoka kwa Mholanzi Sifan Hassan.

Amefichua hayo akiwa mjini Doha, Qatar ambako atatimka katika mbio za 1,500m katika duru ya kwanza ya Ligi ya Almasi hapo Mei 6.

Mholanzi Sifan alinyakua taji la London Marathon katika shindano lake la kwanza la umbali wa kilomita 42 hapo Aprili 23.

Mzawa huyo wa Ethiopia alifyatuka zikisalia chini ya mita 100 na kutawala London Marathon kwa saa 2:18:33, akifuatiwa na Muethiopia Alemu Megertu (2:18:37) na bingwa wa Olimpiki kutoka Kenya, Peres Jepchirchir (2:18:38).

Akizungumza Mei 4, Chepng’etich alisema kuwa ushindi wa Sifan ni motisha kubwa kwake.

“Sifan Hassan alijitahidi kadri ya uwezo wake mjini London. Sikutarajia kabisa. Nataka pia kufanya hivyo, kukimbia marathon siku za usoni. Ushindi wa Sifan ulinipa motisha tele,” alisema mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

Chepng’etich bado anashiriki mbio za uwanjani zaidi, ingawa Februari alitawala mbio za nyika za kilomita 10 za Sirikwa mjini Eldoret.

Baada tu ya Olimpiki mwaka 2021, Chepng’etich alitangaza kuwa ataanza kushiriki mbio za 5,000m. Hata hivyo, amekuwa bado akitetemesha katika 1,500. Atashiriki 1,500 mjini Doha.

  • Tags

You can share this post!

Omanyala kutolewa jasho na Waamerika Kip Keino Classic

Baunsa taabani kwa kumjeruhi mteja klabuni

T L