• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
Benki ya Equity yaingia kwa mkataba wa kibiashara na Tatu City

Benki ya Equity yaingia kwa mkataba wa kibiashara na Tatu City

NA LAWRENCE ONGARO

BENKI ya Equity imefanya ushirikiano na Tatu City kwa lengo la kuendesha biashara ya ununuzi wa majumba katika eneo hilo.

Benki hiyo itakuwa na majukumu ya kuendesha biashara za kibinafsi za wakazi wa Tatu City, kuagiza mikopo, na ununuzi wa mashamba.

Mkurugenzi na mwanzilishi wa Tatu City Bw Stephen Jennings alisema ushirikiano huo ni muhimu kwa wanaomiliki majumba makubwa na wakazi wa eneo hilo kwa sababu watapata pahali pa kuhifadhi fedha zao.

“Lengo letu kuu ni kuona ya kwamba kila mmoja anayeishi sehemu hii anapata mambo kuwa rahisi kwake kwa kuweka fedha kwa benki ya Equity.

Bw Humphrey Muturi, ambaye ni mkurugenzi wa kibiashara wa Benki ya Equity, alisema ushirikiano wao na Tatu City ni mwamko mpya kwa kuendeleza uchumi na kutoa mwelekeo ufaao kwa wafanyabiashara wengi.

“Tunalenga kuinua uchumi wa eneo la Tatu City kwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa kila mmoja,” alisema Bw Muturi.

Kwa wakati huu, wafanyakazi wapatao 9,000 hufanya kazi katika sehemu ya Tatu City huku biashara 75 zikiendeshwa katika eneo hilo.

Baadhi ya biashara zilizoko ni kampuni ya Dormans, Copia, Cooper K-Brands, Grit Real Estate, Income Group, Twiga Foods, Freight Forward Solutions, Friendship Group, Davis & Shirtliff, na Kenya Wine Agencies.

Kuna shule za Crawford International School, na Nova Pioneer ambazo zina wanafunzi wapatao 3,500.

Watu wapatao 4,000 wanaishi katika nyumba za Unity Homes eneo la Kijani Ridge.

Tatu City inashikilia eneo la ekari 5,000 na watu zaidi ya 250,000 wanaishi humo ndani.

Benki ya Equity, mbali na Kenya, ina matawi mengine katika mataifa ya Rwanda, Uganda, Tanzania, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Ethiopia.

Benki hiyo pia inatambulika kwa ubora wake wa huduma na imepata wateja wengi kutoka maeneo mengi duniani.

  • Tags

You can share this post!

Mzee mchimbaji wa madini ya thamani asema cha kujivunia ni...

Serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu yakabidhiwa maktaba ya...

T L