• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Bunge la Kenya na la Hungary kuimarisha ushirikiano, asema Wetang’ula

Bunge la Kenya na la Hungary kuimarisha ushirikiano, asema Wetang’ula

NA BENSON MATHEKA

BUNGE la Kenya na la Hungary zitaimarisha ushirikiano kwa lengo la kunufaisha nchi hizo mbili.

Hii ni baada ya Spika wa Bunge la Taifa Dkt Moses  Wetang’ula, kumwalika mwenzake wa Hungary, Laszlo Kover kuzuru Kenya kwa mazungumzo

Spika huyo wa Bunge la Hungary, yuko nchini kwa ziara rasmi ya wiki moja.

Bw Wetang’ula alishukuru serikali ya  Hungary kwa kutoa ufadhili wa masomo kwa Wakenya zaidi ya  200 hatua ambayo alisema itasaidia kubadilisha maisha ya watu kupitia elimu spesheli na ujuzi.

Spika  Wetag’ula pia alishukuru serikali ya Hungary kwa kusaidia Kenya katika miradi tofauti akisema nchi hizi mbili zina uhusiano wa miaka mingi.

Kuhusu ushirikiano wa Bunge, Bw Wetang’ula alisema utasaidia nchi zote mbili kubadilishana ufahamu na mawazo katika biashara, Kilimo, Elimu, Tekinolojia, Usalama na Utalii.

“Ushirikiano wa Bunge na Bunge ni muhimu kwa ushirikiano wa nchi na nchi katika mipango tofauti ikiwemo kufanya biashara kwa kuwa Kenya inalenga kupanua ushirikiano wa kibiashara,”  akasema Wetang’ula alipompokea Kover katika majengo ya Bunge.

Akisema ni Spika wa kwanza wa Bunge la Hungary kuzuru Kenya kwa ziara rasmi, Laszlo Kover alisema mabunge yana jukumu muhimu kutia nguvu uhusiano wa nchi mbili na akahimiza wabunge kuendelea kuzungumza kuhusu mipango ya maendeleo.

  • Tags

You can share this post!

Ruto na Raila wang’ang’ania Magharibi

Wanafunzi sasa wanywa uji shuleni kupitia mpango wa Soko...

T L