• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:00 PM
COVID-19: Kenya yathibitisha visa vipya 105 na kufikisha 104,306 idadi jumla

COVID-19: Kenya yathibitisha visa vipya 105 na kufikisha 104,306 idadi jumla

Na CHARLES WASONGA

WATU 105 zaidi wamepatikana na virusi vya corona nchini Kenya ndani ya muda wa saa 24 zilizopita.

Kulingana na taarifa iliyotumwa Jumatatu kwa vyombo vya habari na Wizara ya Afya, visa hivyo vipya vya maambukizi vilipatikana baada ya sampuli kutoka kwa watu 3,573 kupimwa.

Idadi jumla ya visa vya maambukizi nchini kuanzia Machi 13, 2020, sasa imefika 104,306 baada ya jumla sampuli 1,269,346 kupimwa.

“Kwa bahati mbaya, wagonjwa wanne zaidi walifariki kutokana na ugonjwa huo na hivyo kufikisha idadi jumla ya wale ambao wameangamia kufikia sasa kuwa 1,827,” ikasema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe.

Jumla ya wagonjwa 49 walithibitishwa kupona ndani ya muda wa saa 24 zilizopita na hivyo kufikisha idadi jumla ya waliopona kufikia Jumatatu kuwa 85,626.

“35 kati yao walikuwa wanatunzwa nyumba ilhali 15 walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini,” taarifa hiyo ikasema.

Wizara hiyo ilisema kuwa jumla ya wagonjwa 333 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini wakitibiwa corona huku wengine 1,281 wakihudumiwa chini ya Mpango wa Utunzwaji Nyumbani.

  • Tags

You can share this post!

WHO yataka serikali ya Tanzania ifichue takwimu za corona

Raia wa Burundi na Mali wamlaghai Mlebanon Sh7m