• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 2:21 PM
Raia wa Burundi na Mali wamlaghai Mlebanon Sh7m

Raia wa Burundi na Mali wamlaghai Mlebanon Sh7m

Na RICHARD MUNGUTI

RAIA wa Burundi na mwingine kutoka Mali walishtakiwa Jumatatu kwa kumlaghai raia wa Lebanon zaidi ya Sh7milioni wakimdanganya watamuuzia kilo 20 za dhahabu.

Mabw Chris Mugisha ( raia wa Burundi) na Bachiry Mohamed almaarufu Abdoulay Bashir kutoka Mali walishtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Nairobi Bi Martha Mutuku kwa ulaghai.

Wawili hao walikanusha shtaka mnamo Feburuari 17, 2021 katika mtaa wa Kilimani Nairobi wakiwa na nia ya kulaghai walipokea Dola za kimarekani ($) 64,500 (KSh7,095,000) kutoka Bw Hwalla Karim wakidai walikuwa na uwezo wa kumuuzia kilo 20 za dhahabu.

Mahakama ilifahamishwa wawili hao walimdanganya Bw Karim watasafirisha kwa ndege dhahabu hiyo kwa ndege hadi mjini Beirut nchini Lebanon.

Bw Bashir alikabiliwa na shtaka la kupatikana nchini bila vyeti vya kumruhusu kuishi nchini Kenya.

Huku akitokwa na jasho jingi , Bw Bashir alimweleza hakimu kwamba alikuwa na Visa ambayo muda wake umeyoyoma lakini amepewa jingine ya muda kutoka Ubalozi wa Mali nchini Ethiopia inayomruhusu kusafiri hadi nchini Kenya.

Wakili Stanley Kang’ahi anayewakilisha wawili hao alieleza mahakama kwamba “Pasipoti ya Bw Bashir ikon a Visa hiyo ya kumwezesha kuingia na kuishi nchini.”

Bw Kang’ahi aliomba waachiliwe kwa dhamana.

Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda alieleza korti hapingi washtakiwa wakiachiliwa kwa dhamana.

Bi Mutuku aliamuru kila mmoja wa hao wawili alipe dhamana ya pesa tasilimu Sh500,000 kabla ya kuachiliwa kutoka kizuizini.

Hakimu aliamuru kesi hiyo itajwe tena Machi 8,2021 upande wa mashtaka ueleze ikiwa umewakabilidhi washtakiwa nakala za ushahidi.

  • Tags

You can share this post!

COVID-19: Kenya yathibitisha visa vipya 105 na kufikisha...

Raia wa TZ akana kuuza vifaa feki vya kupima Ukimwi Kenya