• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:09 AM
Maafisa wa DCI wamkamata mwanamume anayeshukiwa kumuua kinyama mpenziwe wa zamani, Kayole wiki jana

Maafisa wa DCI wamkamata mwanamume anayeshukiwa kumuua kinyama mpenziwe wa zamani, Kayole wiki jana

Na CHARLES WASONGA

MWANAMUME anayeshukiwa kumuua mpenziwe kwa kumfunga kwenye kitanda na kumteketeza amepatikana na maafisa wa upelelezi wa jinai.

Tayari Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imethibitishwa kuwa maafisa wake wamefaulu kumkamata mwanamume anayeshukiwa kumuua mpenziwe za zamani kwa kuteketeza ndani ya nyumbani yake (marehemu) Alhamisi wiki jana, katika eneo la Njiru, Nairobi.

Kwenye taarifa kupitia Twitter, DCI inasema wapelelezi walimpata mshukiwa huyo akiwa amejifungia katika chumba moja kwenye jumba la orofa tano mtaani Kayole Nairobi.

“Hatimaye maafisa wetu wamefaulu kumshawishi asijiue na wamemkata kwa lengo la kumshtaka kwa mujibu wa sheria kwa kutenda kosa hilo la kinyama,” DCI ikaeleza.

Awali katika ujumbe kupitia akaunti yake ya Twitter, (DCI) Jumatano imesema kuwa mshukiwa huyo ambaye amekuwa akisakwa tangu wiki jana, alikuwa amejifungia katika chumba kimoja katika orofa ya tano ya jengo la makazi mtaani Kayole, Nairobi.

“Wakati huu yuko katika roshani ‘balcony’ akitisha kujitoa uhai. Maafisa wetu wanambembeleza asijiue kwa sababu ya matendo yake kwani ataweza kupata suluhu ya tatizo linalomzonga,” ikasema DCI.

Inaripotiwa kuwa marehemu, Margaret Muchemi, alikuwa amemwalika mshukiwa huyo waliyetengana zamani, nyumbani kwake ili wazungumzie masuala yaliyosababisha tofauti kati yao.

Wajakazi wawili wa marehemu waliwaambia polisi kuwa mshukiwa aliwasili mwendo wa saa mbili za asubuhi Alhamisi na bosi wao akawaambia wawape “ajadiliane suala muhimu faraghani na mpenzi wake wa zamani.”

“Baadaye majira ya adhuhuri moto ulionekana katika nyumba hiyo na juhudi za majirani kuuzima au kuokoa marehemu hazikufua dafu,” DCI ikasema.

Uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa mikono na miguu ya marehemu, iliyochomeka, ilionekana kama ambayo ilikuwa imefungwa kwenye kitanda kabla ya mwili wake kuteketezwa. Uso wake pia ulikuwa umeteketea kabisa.

Marehemu Muchemi, 34, ambaye ni mama wa mtoto mmoja, ambaye alikuwa ni tabibu, alikuwa akiendesha kliniki moja katika mtaa wa Mwiki, Kasarani, Nairobi.

  • Tags

You can share this post!

VITUKO: Pengo alaghaiwa na mwanafunzi mjanja kuvunja amri...

Raila atarajiwa Githurai kupigia debe BBI