• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Demokrasia yazidi kunawiri Kenya, asema mkurugenzi wa MPC

Demokrasia yazidi kunawiri Kenya, asema mkurugenzi wa MPC

Na SAMMY KIMATU

WAKENYA wameonyesha ulimwengu wote wamekua kidemokrasia kwa kuonyesha utulivu na kudumisha amani kabla, wakati wa uchaguzi na kipindi cha baada ya uchaguzi uliofanyika Agosti 09, 2022, amesema Mkurugenzi wa Shirika lisilo la serikali la Mukuru Promotion Centre (MPC) mtawa Mary Killeen.

Aidha alisema siku zijazo, iwapo sheria itaruhusu, itakuwa muhimu kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kufanya uchaguzi mwezi Disemba.

Aliongea hayo alipokutana na wageni wanaofadhili elimu ya watoto kutoka familia maskini maeneo ya Mukuru katika Kituo cha Watoto Walemavu cha Songa Mbele na Masomo.

Mtawa Killeen alisema ni vyema uchaguzi kufanyika Disemba wakati shule zote zimefungwa bila kuhitilafiana na kalenda ya elimu.

“Watoto walilazimika kubaki nyumbani kwa siku kadhaa kupisha shughuli ya uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwezi huu. Ni bora chaguzi kuratibiwa Disemba wakati shule zote nchini huwa zimefungwa kwa shamrashamra za Krismasi na Mwaka Mpya,” Mtawa Killeen akasema.

Isitoshe, Mtawa Killeen alipongeza Huduma ya Polisi Nchini akisema maafisa wa polisi walidhibiti usalama bila kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa uchaguzi uliomalizika.

Bali na hayo, aliongeza kwamba kinyume na wali wakenya walipoandamana barabarani kupinga matokeo ya kura ya rais, wakati huu wanatumia Korti ya Upeo.

“Wakenya wamekomaa kisiasa. Leo wamefika kortini kupeleka malalamishi yao tofauti na miaka mingine watu wakipoteza maisha yao kufuatia fujo na ghasia za baada ya kutangazwa kwa kura ya utrais,” Mtawa Killeen akasema.

  • Tags

You can share this post!

Moraa mbioni kuwa Mkenya wa kwanza mwanadada kutimka mbio...

Serikali yaahidi uwajibikaji kufuatia shambulio lililoua 21

T L