• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
Moraa mbioni kuwa Mkenya wa kwanza mwanadada kutimka mbio fupi Diamond League

Moraa mbioni kuwa Mkenya wa kwanza mwanadada kutimka mbio fupi Diamond League

NA AYUMBA AYODI

BINGWA wa michezo ya Jumuiya ya Madola mbio za mita 800, Mary Moraa ananusia kuweka historia kwenye riadha za Diamond League atakapotimka mita 400 mjini Brussels, Ubelgiji mnamo Septemba 2.

Hakuna mwanamke kutoka Kenya amewahi kushiriki mbio fupi kwenye Diamond League, na Moraa, ambaye anashikilia rekodi ya 400m, tayari anasubiri kwa hamu kubwa.

Moraa, 22, anayeorodheshwa nambari 26 duniani msimu huu katika 400m kwa sekunde 50.84, alisema analenga kutumia mbio hizo za kuzunguka uwanja mara moja kutafuta kasi kabla ya fainali ya 800m mnamo Septemba 7-8 nchini Uswisi.

“Nimerejea mazoezini baada ya michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Birmingham. Mbio za mzunguko mmoja ni za kufungua tu mwili wangu kwa nia ya kupata kasi,” alisema Moraa anayelenga kuimarisha muda wake bora katika 400m wa sekunde 50.84 na mita 800 wa dakika 1:56.71.

“Nitafurahi sana nikinyoa sekunde kadhaa katika 400m na pia 800m,” alisema.

Hakuna Mkenya ameshinda taji la Diamond League mbio za 800m tangu Eunice Sum mwaka 2015.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

You can share this post!

Wizara yaondolea wazazi hofu kuhusu Gredi 7 chini ya CBC

Demokrasia yazidi kunawiri Kenya, asema mkurugenzi wa MPC

T L