• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Dereva wa matatu mashakani kwa kuharibu ‘radio call’ ya polisi

Dereva wa matatu mashakani kwa kuharibu ‘radio call’ ya polisi

NA RICHARD MUNGUTI

DEREVA wa matatu ameshtakiwa kwa kumnyang’anya kimabavu afisa wa polisi redio yake ya mawasiliano (radio call) na kuiharibu.

Edwin Thairu Njoroge aliyeshtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bi Esther Kimilu alikana mashtaka mawili aliyofunguliwa na Afisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma (ODPP).

Shtaka la kwanza lilikuwa la wizi wa kimabavu na la pili lilikuwa la kuharibu mali ya serikali.

Katika shtaka la kwanza, Njoroge alishtakiwa kwa kumnyang’anya kimabavu afisa wa polisi Idara ya Trafiki, Konstebo Stanley Chege kifaa rasmi cha polisi cha mawasiliano.

Njoroge alidaiwa alitekeleza uhalifu huo mnamo Oktoba 3, 2023 katika barabara ya General Mathenge eneo la Westlands, Nairobi.

Mshtakiwa alidaiwa alikuwa amejihami kwa vipande vya fito vya chuma.

Katika eneo la Sir George, Kaunti ya Kiambu Njoroge alidaiwa ndiko alifanya uharibifu wa redio hiyo ya polisi.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500, 000.

Kesi hiyo itatajwa Oktoba 23, 2023.

 

  • Tags

You can share this post!

Raia wa Tunisia aliyepatikana na pesa feki atakiwa kortini...

Ajabu ya hedhi za wanawake kuwa na njama ya kuchocheana

T L