• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 6:39 PM
Raia wa Tunisia aliyepatikana na pesa feki atakiwa kortini mara moja

Raia wa Tunisia aliyepatikana na pesa feki atakiwa kortini mara moja

NA RICHARD MUNGUTI

MSHUKIWA mkuu katika kesi ya kashfa ya dhahabu ya Sh1 bilioni iliyomuhusisha raia wa Tunisia ameagizwa ajisalamishe kortini mnamo Oktoba 18,2023 kujibu nashtaka ya kupatikana na pesa feki USD ($) 634,178 (KSh 93, 477, 837).

Na wakati huo huo hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bi Esther Kimilu alimwagiza afisa wa polisi anayechunguza kesi hiyo abaini ikiwa Joseph Lendrix Waswa amekuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya MP Shah.

Bi Kimilu alitoa agizo hilo baada ya kuombwa na wakili June Ashioya aahirishe kesi inayomkabili Bw Waswa kwa muda wa siku 60 kumwezesha kupata matibabu maalum.

“Mshtakiwa hajafika kortini leo (Oktoba 9, 2023) kwa vile anapokea matibabu maalum katika hospitali ya MP Shah,” Bi Ashioya alimweleza hakimu.

Wakili huyo alimkabidhi hakimu rundo la karatasi za matibabu kutoka hospitali ya MP Shah anakolazwa Bw Waswa.

Bi Ashioya aliomba korti imruhusu mshtakiwa muda apone kisha afike kortini kujibu shtaka.

Lakini ombi hilo lilipingwa vikali na kiongozi wa mashtaka Bi Anne Munyua.

Bi Munyua alisema, “Naomba hii mahakama iamuru afisa anayechunguza kesi hii afike katika Hospitali ya MP Shah kubaini matibabu anayopokea.”

Pia kiongozi huyo wa mashtaka alisema wiki mbili zilizopita Bi Ashioya aliwasilisha ripoti kortini kwamba Bw Waswa alikuwa amepewa maagizo apumzike lakini “sasa mambo yamebadilika.”

Bi Munyua aliomba ripoti kumhusu Bw Waswa iwasilishwe kortini.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Pigo kwa Ruto mpango kupeleka askari 1, 000 Haiti ukizimwa...

Dereva wa matatu mashakani kwa kuharibu ‘radio call’ ya...

T L