• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Familia yapinga mshukiwa wa mauaji ya baba yake kupewa dhamana

Familia yapinga mshukiwa wa mauaji ya baba yake kupewa dhamana

NA BRIAN OCHARO

MWANAMUME aliyeshtakiwa kwa madai ya kumuua baba yake na kuficha mwili wake kwa gunia, atasalia rumande hadi kesi itakapokamilika, baada ya familia yake kupendekeza hivyo.

Familia ya Abdul Majid Nagil, 28, ambaye amehusishwa na mauaji ya Nagis Abdallah Fateh, 69, ilipendekezea mahakama kuwa, hafai kupewa dhamana kwa kuwa anaweza kutoroka.

Ripoti kuhusu tabia ya mshukiwa iliyowasilishwa mahakamani, ilionyesha kuwa familia hiyo pia ilisema huenda akavamiwa na jamii ambayo bado ina hasira naye.

“Wanahisi kwamba ikiwa ataachiliwa kwa dhamana, anaweza kuchomwa kwa kuwa jamii ina hasira naye kutokana na kitendo anachohusishwa nacho. Familia pia inahofia kwamba kwa vile (Majid) amekuwa akiishi nje ya nchi, anaweza kutoroka kwa urahisi bila kujulikana hivyo basi kuhujumu kupatikana kwa haki,” ripoti hiyo ilisema.

Kutokana na uchunguzi uliofanywa na polisi, mtuhumiwa ameishi Dubai kwa muda mrefu na pia ana jamaa zake wanaoishi nje ya nchi.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Mombasa, Bi Anne Ong’injo, aliamua kulikuwa na sababu za kutosha za kumnyima dhamana Bw Majid hadi kesi itakapoamuliwa.

Mahakama ilikataa pendekezo lake la kuhamia Juja, Kaunti ya Kiambu ambako ana marafiki zake ikibainika kuwa alikosa kufichua marafiki hao ni kina nani na kwamba marafiki hao hawakuweza kupatikana kwa ajili ya mahojiano.

Mauaji yalitokea Mombasa mwaka 2021 katika mtaa wa Bondeni.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Si lazima lugha ya mama iwe ya kugawanya raia wa...

Vijana wakosolewa kupenda bodaboda badala ya masomo

T L