• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 8:11 PM
TAHARIRI: Si lazima lugha ya mama iwe ya kugawanya raia wa nchi

TAHARIRI: Si lazima lugha ya mama iwe ya kugawanya raia wa nchi

NA MHARIRI

JUMATATU wiki hii, ulimwengu uliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilipongoza maadhimisho hayo kwa mada “Utumizi wa Teknolojia kujifunza lugha mbalimbali: Changamoto na Fursa zake.”

Lugha hutekeleza jukumu muhimu katika maendeleo, kuhakikisha kuna tamaduni mbalimbali, na pia huimarisha ushirikiano miongoni mwa mambo mengine ya mwsingi.

Takwimu zinaonyesha kuwa wakati shule zilipofungwa kutokana na janga la Covid-19 kote ulimwenguni, mataifa mengi yalitumia teknokojia kuendeleza masomo.

Hapa Kenya, kwa mara ya kwanza wanafunzi katika shule za umma walianza kusoma kupitia mitandao kama Zoom.

Lakini wengi, hasa maeneo ya mashambani walibaki nyumbani bila kusoma, kutokana na ukosefu wa vifaa kama simu, kompyuta, mtandao wa intaneti na hata watu wa kuwafunza.

Katika mataifa kama China, Bangladhesh na mengine ya Mashariki ya Mbali, wanafunzi wengi walipata maarifa makubwa wakati huo kutokana na utumizi wa lugha za mama.

Rais Uhuru Kenyatta amekuwa akionyesha mfano kwa kuwasiliana na watu wa eneo la Mlima Kenya kwa lugha ya mama.

Labda hii inatokana na kauli ya Nelson Mandela kwamba, “Ukitaka mtu afahamu unachosema, tumia lugha anayoijua. Lakini ukitaka maneno yamwingie moyoni, tumia lugha yake.”

Lugha ya mama ni chombo muhimu kwa jamii yoyote.

UNESCO inaonyesha kwamba karibu nusu ya lugha 6,000 zinzozungumza duniani zipo katika hatari ya kuangamia.

Lugha hizi zinaweza kuhifadhiwa kwa kuweka mikakati ya kuwafunza watoto wakiwa katika umri mdogo.

Watu wengi wanaoishi mijini au walio katika ndoa za kuchanganya kabila, huwa hawaoni umuhimu wa kuwafunza watoto wao angalau lugha ya mmoja wao au za wote wawili.

Kuijua lugha si lazima iwe chanzo cha watu kuchukia watu wasiozungumza lugha yao.

Serikali kupitia mfumo wa CBC, inapaswa kufikiria upya jinsi ya kuwezesha watoto wanaoishi kwenye miji wanaweza kufunzwa lugha zao za asili.

Ingawa linaonekana kuwa jambo gumu kutelezeka, linawezekana.

Badala ya kuweka sehemu tu ya mafunzo kama vile utamaduni, vyakula, mavazi na kadhalika, mtaala wa CBC yafaa usisitize pia wazazi kuwafunza watoto wao lugha ya mama.

Ni kwa njia hii ambapo Kenya itakuwa na watu wanaothamini mambo ya kimsingi yanayochukuliwa na wengi kuwa yasiyokuwa na umuhimu.

You can share this post!

VALENTINE OBARA: Kuna kila ishara uchaguzi mkuu ujao huenda...

Familia yapinga mshukiwa wa mauaji ya baba yake kupewa...

T L