• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Gachagua arejea nchini kimya kimya na kuongoza mkutano mdogo wa Baraza la Mawaziri

Gachagua arejea nchini kimya kimya na kuongoza mkutano mdogo wa Baraza la Mawaziri

NA LABAAN SHABAAN

NAIBU Rais Rigathi Gachagua ameongoza mkutano mdogo wa baraza la mawaziri Jumatano, Novemba 1, 2023 baada ya kurejea nchini kimya kimya Jumanne usiku.

Yamkini Naibu Rais aliingia nchini kutoka ziara yake ya Ulaya baada ya wakosoaji wake mitandaoni kumshambulia kwa kukosa dhifa ya Ikulu.

Bw Gachagua hakuhudhuria dhifa ya Mfalme wa Uingereza Charles III na Malkia Camilla Jumanne usiku Oktoba 31, 2023 kwa sababu alikuwa safarini Ulaya.

Waliomshambulia mitandaoni walimkejeli eti alishindwa kumzuia Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kuingia Ikulu: Bw Odinga alishiriki dhifa hiyo ya kifalme pamoja na viongozi wengine waalikwa.

Baada ya kurejea, Naibu Rais alikuwa mwenyeji wa mkutano mdogo wa mawaziri katika afisi yake ya Karen.

Mkutano huo uliangazia mikakati inayotumiwa kufanikisha ajenda ya kustawisha uchumi ya Bottom – Up.

“Leo nilikuwa mwenyekiti wa mkutano wa Kamati ya Baraza La Mawaziri katika afisi yangu ya Karen, Nairobi. Mkutano huu unatuwezesha kufanyia ukarabati mikakati ya kuimarisha uchumi ili kuafikia utoaji huduma bora,” alisema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X.

Bw Gachagua alikosa kuonekana katika siku ya kwanza ya ziara ya Mfalme wa Uingereza aliyewasili nchini Jumatatu jioni mnamo Oktoba 30, 2023 kwa safari ya siku nne.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamuziki Ali Khamis almaarufu Ally B aaga dunia

Nimerudi soko, atangaza Akothee akithibitisha kwa mara ya...

T L