• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 3:57 PM
HIVI PUNDE: Serikali yakubali kuongezea walimu mshahara

HIVI PUNDE: Serikali yakubali kuongezea walimu mshahara

NA DAVID MUCHUNGUH

WALIMU ni miongoni mwa watumishi wa umma watakaokuwa na tabasamu hivi sasa baada ya serikali kukubali nyongeza yao ya mishahara ya kati ya asilimia 7 na 10.

Haya yanajiri huku awali ripoti zikisema kwamba mishahara yao ya Agosti itachelewa kwa kutegemea matokeo ya mazungumzo kati ya vyama vyao na mwajiri wao, Tume ya TSC, yaliyokuwa yanaendelea leo Agosti 28, 2023.

TSC kufikia Jumapili Agosti 27, 2023 haikuwa imetoa taarifa za mshahara wa walimu huku ikisubiri kuona iwapo itafikia muafaka na vyama vya kuwatetea baada ya mazungumzo ya awali kugonga mwamba wiki iliyopita.

Walimu waliozungumza na Taifa Leo Jumapili walisema kwamba hawajapata taarifa zao za mishahara katika tovuti ya TSC jambo ambalo sio kawaida.

Kufuatia pande zote kukubaliana, walimu watapata nyongeza hiyo katika miaka miwili huku mkataba huo ukiongezwa kwa ule unaoendelea wa makubaliano ya pamoja (CBA) ya 2021-2025.

  • Tags

You can share this post!

Raila motoni kwa kutishia kurejelea maandamano

Mwili wa mwanamume wapatikana kwenye tanuri la uchomaji...

T L