• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Hospitali ya KNH yasema itatupa miili 253 jamaa wasipojitokeza kuichukua

Hospitali ya KNH yasema itatupa miili 253 jamaa wasipojitokeza kuichukua

NA MERCY KOSKEI

HOSPITALI ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) imetangaza kutupa miili ambayo haijachukuliwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti iwapo jamaa zao watakosa kufika na kuitambua katika muda wa siku saba zijazo.

Kulingana na notisi kutoka hopitali hiyo, miili 253 hazijachukuliwa na kati ya miili hizo 239 ni za watoto ikifichua kuwa iwapo wapendwa wao hawatawatambua kwa siku hizo saba watazikwa kwa makaburi ya pamoja.

Kupitia notisi hiyo, KNH ilisema kuwa inanuia kuomba idhini kutoka kwa mahakama kabla ya kuziondoa miili hizo.

“Wananchi wanaombwa kufika na kutambua na kuchukua miili hizo ndani ya siku saba, ikishindikana hospitali itatafuta idhini ya mahakama kuzitupa,” notisi ya ilani ilisema.

Kulingana na orodha iliyotolewa na KNH, watoto ndio kundi kubwa lililoathiriwa. Miongoni mwa watoto hao ni seti tano za mapacha na seti ya mapacha wanne.

Wasimamizi wa KNH walibaini kuwa miili ya watu wazima 13 ambao hawajatambuliwa pia imeifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti vya serikali jijini Nairobi.

Miili 11 ni ya kiume 2 ikiwa ya kike.

Hospitali hiyo ilisema orodha ya majina inapatikana katika chumba cha maiti ya KNH na pia inaweza kupatikana kupitia tovuti ya taasisi hiyo.

Mnamo Septemba, KNH ilitupa miili 169 ambayo haikuchukuliwa na jamaa katika hifadhi ya maiti ya city na 24 katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki.

  • Tags

You can share this post!

Mbunge Patrick Makau aitwa na DCI kuhojiwa kuhusu ardhi ya...

Daktari abaini wanafunzi wa Amabuko waliugua kwa kula...

T L