• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Jinsi Gachagua alivyofanya mazoezi ya kutembea asubuhi ya majogoo katika ‘makao makuu ya ingokho’

Jinsi Gachagua alivyofanya mazoezi ya kutembea asubuhi ya majogoo katika ‘makao makuu ya ingokho’

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Rais Rigathi Gachagua amerauka asubuhi na mapema kutembea mjini Kakamega akipata fursa ya kipekee kujionea wakazi wakiendelea na shughuli zao za wikendi.

“Hii asubuhi nimejionea mandhari ya kuvutia katika mji wa Kakamega,” ameandika Naibu Rais kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Amesema amepunga hewa safi kutokana na upekee wa miti mingi na misitu muhimu katika kipindi hiki ambapo dunia inakabiliwa na matatizo ya mabadiliko ya tabianchi.

Naibu Rais Rigathi Gachagua akitembea mjini Kakamega asubuhi ya Jumapili, Agosti 27, 2023. PICHA | HISANI

Bw Gachagua amesema miti mjini Kakamega na viungani mwa mji huo ni kitulizo kamili kwa wenyeji na wageni wanaozuru Magharibi mwa Kenya.

Baadaye Bw Gachagua ameungana na Rais William Ruto aliyehudhuria maombi ya muungano wa makanisa mbalimbali katika uwanja mdogo wa ndege ulioko katika kaunti jirani ya Bungoma.

Baadaye Naibu Rais Rigathi Gachagua amejiunga na Rais William Ruto kwa maombi kwenye uwanja mdogo wa ndege katika Kaunti ya Bungoma. PICHA | ISAAC WALE

Rais Ruto anafanya ziara katika eneo la Magharibi kutangamana na wakazi, ambao wengi ni wa jamii ya ‘Mulembe’.

Naibu Rais Rigathi Gachagua akifanya mazoezi mjini Kakamega mnamo Agosti 27, 2023. PICHA | HISANI
  • Tags

You can share this post!

Kisanga mimba ya mke wa wenyewe kujiavya akigawa tunda la...

Didmus Barasa: Tulipopeleka Raila Bondo, tulipaswa kuweka...

T L