• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Kisanga mimba ya mke wa wenyewe kujiavya akigawa tunda la ndoa kwa ‘mubaba’ lojing’i Murang’a

Kisanga mimba ya mke wa wenyewe kujiavya akigawa tunda la ndoa kwa ‘mubaba’ lojing’i Murang’a

NA MWANGI MUIRURI

MURANG’A

KIZAAZAA kilizuka majuzi Mjini Murang’a baada ya mama aliyekuwa mjamzito mimba kutoka wakati akijiburudisha na mpango wake wa kando kwenye lojing’i.

Tukio hilo linalochukuliwa kama la kuavya mimba, lilishtua wengi wahudumu wa lojing’i hiyo, mmoja akisimulia Taifa leo Dijitali alichoshuhudia.

“Ni jambo la kushtua. Mwanamume na mwanamke, ni walimu wa shule moja ya Kaunti Ndogo Gatanga na walikuwa wamefika katika lojing’i kurushana roho. Mwanamke alikuwa na mimba. Mwendo wa saa tisa, mwanamume alinijia akiwa na taharuki akiniambia kulikuwa na ajali ndani ya chumba chake,” akasema mhudumu wa lojing’i hiyo.

Alisema aliandamana na mwanamume huyo hadi katika chumba hicho, na akakumbana na mwanamke akiwa amepoteza fahamu huku kitanda kikiwa kimelowa damu.

“Mimi nikiwa mwanamke kuna vile niligundua hiki kilikuwa kisa cha mimba kujiavya…Labda walikunjana sana huku wakijituma kwa bidii za mchwa katika harakati za kupiga moyo pasi…Lakini cha maana kilikuwa kutatua hali,” akasema.

Mhudumu huyo alituarifu kwamba aliita daktari rafiki wa lojing’i hiyo ambaye alifika kutoa huduma ya kwanza.

“Daktari alifika na baada ya ng’ang’ana zake, mwanamke alipata fahamu kisha tukaita ambulensi ambayo ilifika na kumpeleka hospitalini alikolazwa,” akasema.

Ripoti ya polisi ambayo iliandaliwa kuhusu kisa hicho ilisema kwamba “Kuna mwanamke wa miaka 24 ambaye aliripotiwa kuugua akiwa katikia chumba cha burudani akiandamana na rafiki yake wa kiume wa miaka 58”.

Ripoti hiyo iliongeza, “Baada ya ripoti za ukaguzi wa utaalamu wa kimatibabu kutekelezwa, ilibainika kwamba mwanamke huyo alipata mkosi wa mimba ya miezi mitano kujiavya, kiini kikitolewa kuwa presha katika chungu cha mwana”.

Kwa kuwa hakuna malalamiko kutoka kwa yeyote kuhusu kisa hicho, ripoti hiyo ilisema hakuna aliyekamatwa “Wote wawili walisema ni marafiki na walikuwa katika harakati zao za amani wakati ajali hiyo ya kiafya iliingia”.

Mhudumu wa lojing’i aliyezungumza na Taifa Leo Dijitali, alielezea hofu yake iwapo vyombo vya habari vitaangazia tukio hilo na kufichua majina ya wahusika mwanamke huyo huenda akawa katika hatari ya kukabidhiwa talaka na mumewe.

Alisema kwamba baada ya mkosi huo, mwanamke huyo alipeana nambari ya simu ya mume wake lakini kukatolewa hongo ya Sh12, 000 ili aambiwe kwamba alikumbwa na matatizo ya kiafya akiwa katika mkahawa na marafiki wa kike.

Cha kushangaza zaidi, ilikubaliwa aelezwe dharura hiyo ililazimu atafutiwe hifadhi ndani ya chumba kimoja cha lojing’i kusubiri ambulensi.

 

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

KINAYA: Gachagua atawaweza nyuki wa Ukambani aliochokoza?

Jinsi Gachagua alivyofanya mazoezi ya kutembea asubuhi ya...

T L