• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Jinsi tunavyoweza kuimarisha umiliki wa vipande vya ardhi, kuvutia vijana kwenye sekta ya kilimo

Jinsi tunavyoweza kuimarisha umiliki wa vipande vya ardhi, kuvutia vijana kwenye sekta ya kilimo

Na SAMMY WAWERU

KUNA haja ya kutathmini mila na itikadi zetu kama Waafrika kuhusu umiliki wa ardhi.

Katibu Mkuu katika Wizara ya Masuala ya Vijana, Bw Charles Sunkuli amesema sekta ya kilimo Afrika itaendelea kujikokota kwa sababu ya mila kali kuhusu umiliki wa mashamba.

Bw Sunkuli amesema mtazamo wa wazazi ndio pekee wanapaswa kumiliki ardhi na kutoa maamuzi ya kilimo, ndio unachangia upungufu wa chakula Afrika.

Amesema, ili kuangazia gapu ya chakula Afrika, idadi kubwa ikiendelea kusakamwa na njaa, ni muhimu vijana wahusishwe katika umiliki wa mashamba na kuendeleza kilimo.

“Mila na itikadi zetu kama Waafrika zimewapa wazazi mamlaka makuu kumiliki mashamba na kuamua kinachopaswa kulimwa. Haja ipo tuzitathmini ikiwa tunataka kuboresha kilimo,” akasema.

Kwa vijana wenye ari kujiendeleza kilimo, ila hawana kipande cha ardhi, Bw Sunkuli alisema mila zimewazuia kukiboresha.

“Kuna vijana wenye maono, wangetaka kuimarisha kilimo kwa kukuza mimea ya thamani. Wangekuwa na mashamba wangesaidia katika mchango wa kuwepo kwa chakula cha kutosha,” akaelezea.

Katibu Sunkuli alisema kinachofanya mataifa ya ughaibuni kubobea katika shughuli za kilimo na kuwa na chakula cha kutosha ni kuwapa vijana ardhi, na kuwaruhusu kukuza mimea wanayotaka.

“Mambo yanakua kiteknolojia, na vijana wanaielewa. Mchango wa vijana katika kilimo usipuuzwe,” akahimiza.

You can share this post!

Mashindano ya Cecafa ya kina dada yaahirishwa hadi Agosti,...

Polisi wakanusha kujua aliko mwanamume aliyetoweka Lamu...