• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 5:59 PM
Jombi atozwa Sh30, 000 kwa kugusa uchi wa mwanamitindo

Jombi atozwa Sh30, 000 kwa kugusa uchi wa mwanamitindo

NA MWANGI MUIRURI 

Murang’a Mjini

POLO katika baa moja ya hapa ambayo wanawake hunengua viuno wakiwa uchi alipata mshtuko si haba alipotozwa faini ya Sh30, 000 kwa kupapasa makalio ya mmoja wao.

Sheria huwa usijaribu kugusa sehemu yoyote hata akija karibu nawe ikiwa hamujaelewana na msikizane bei.

“Kwa kawaida, ukimpa mrembo huyo Sh500 huwa anakubali umpapase makalio huku Sh1, 000 ikikupa idhini ya kugusagusa kwingineko ikiwemo nyeti…Sh200 unaweza ukapewa busu huku Sh100 zikikupa ruhusa ya kukumbatiwa,” akasema bawabu wa baa hiyo.

Sh2, 000 huwa ni gharama ya kukaliwa ukiwa huzimiwi raha huku Sh3,000 zikitosha umtoroshe hadi utakako.

“Lakini polo na ulevi wake aliamua kujigawia raha na ndipo akamvuta mmoja wa wanenguaji hao na akamkumbatia, akampiga busu na akamfinyafinya kana kwamba alikuwa akitaka kujua parachichi limeiva,” akasema mdokezi.

Kizazaa kiluzuka huku mrembo huyo akiteta kukiukwa kwa sheria za kikazi na ndipo wasimamizi wakaingilia kati.

Licha ya polo kujitetea kwamba yeye ni mteja wa kila siku ndani ya baa hiyo inayomilikiwa na bwanyenye fulani, iliamuliwa kwamba nidhamu ni ya maana na ni lazima angelipa fidia.

“Polo alijaribu kujitetea kwamba hakuna sheria inayoruhusu mtu kuchapa densi mbele yake akiwa uchi na alikuwa akimsukuma mrembo huyo ili amwondokee lakini malilio yake yakaambulia pakavu,” bawabu akasema.

Ni wakati ambapo meneja wa baa hiyo alimtisha kwamba angeita maafisa wa polisi ili akamatwe kwa makosa ya unyanyasaji wa kijinsia na pia amfahamishe bibi ya polo kuhusu kisa hicho ambapo hata ndiye aliamua kulipa Sh30, 000.

“Anajulikana vyema hapa mjini kwa kuwa anafanya kazi katika serikali ya kaunti. Aliogopa sana kisa hicho kufanywa kuwa kesi na pia kuanikwa kwa familia yake…Aliapa kwamba hakuna wakati mwingine atawahi kuwa mteja wa baa hiyo,” akasema meneja wa baa hiyo.

 

[email protected]

 

 

 

  • Tags

You can share this post!

Waziri Namwamba aonya maafisa wasiofaa

Ruto akitaka anapata

T L