• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
‘Kaeni chonjo watoto wasiingie kwa baa’

‘Kaeni chonjo watoto wasiingie kwa baa’

NA MWANGI MUIRURI

KAMATI ya usalama katika eneo la Mlima Kenya imetoa amri kwa maafisa wa usalama wazime visa vya watoto kuwa wateja ndani ya baa za eneo hilo.

“Visa vyote vya watoto kufika katika baa kununua pombe na hatimaye kujiingiza kwa ngono katika madanguro vizimwe kwa nguvu zote za kisheria,” ilani ya Mshirikishi wa eneo la Kati Bw Fred Shisia yasema.

Aidha, mikesha yote ya kupisha Krismasi ni marufuku huku akisisitiza kwamba mkesha wa Mwaka Mpya utafanyika kwa masharti atakayotoa mnamo Desemba 30, 2023.

“Ulevi na mahaba kwa watoto huondoa heshima za taifa kupitia mimba na ndoa haramu pamoja na magonjwa. Hali zote hizi zikichangia upumbavu wa kutosoma miongoni mwa watoto, hasa wa kike mashinani,” akasema Bw Shisia katika ilani hiyo ya Desemba 23, 2023.

Bw Shisia pia alizitaka kamati zote za kiusalama mashinani ziwajibikie doria za kina kuzima baa za kukiuka sheria, magenge kutesa, mangweni ya vileo haramu na mihadarati pamoja na hatari nyingine zozote za kuhujumu usalama kwa vyovyote vile.

“Hata hivyo, doria hizo ni lazima ziwe na uwajibikaji na zisitumiwe kuzua hofu na mahangaiko dhidi ya wasio na hatia,” akasema.

Amewaonya maafisa dhidi ya kuitisha hongo na kuwadhulumu raia.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Chapati Festival: Krismasi ya mapema Riruta

Mwanajeshi, mpenziwe ndani kwa wizi wa bastola

T L