• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:55 AM
Kampuni ya Thiwasco yapanda miti 1,500 Kang’oki kuvutia nyuni wa angani

Kampuni ya Thiwasco yapanda miti 1,500 Kang’oki kuvutia nyuni wa angani

KAMPUNI ya  maji ya THIWASCO imefanya juhudi na kupanda miti 1,500 katika eneo la Kang’oki Sewage mjini Thika.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw Moses Kinya alisema kampuni hiyo inataka kuwa mstari wa mbele katika uhifadhi wa mazingira hasa katika eneo hilo.

“Tunataka kuona ya kwamba eneo hili linabadilika pakubwa ambapo baada ya muda fulani liwe na mazingira ya kutamanika,” alisema Bw Kinya.

Alieleza kuwa eneo hilo linavutia aina 6,000 za ndege wa kutoka sehemu tofauti ulimwenguni na ndiyo maana ni muhimu kupanda miti.

Alisema hivi karibuni wasomi wengi watalazimika kuzuru eneo hilo ili kuchunguza na kufahamu umuhimu wa ndege hao kuzuru hapo.

Alitaja eneo hilo kama la ekari 130 ambapo linahudimia wakazi wa Thika kwa kuhifadhi maji taka na kuyaweka dawa ili kupunguza harufu mbaya.

“Hii sehemu ni muhimu sana kwa sababu inategemewa na watu wengi kwa kuhifadhi maji taka yote inayotumika mji wa Thika na vitongoji vyake,” alifafanua mkurugenzi huyo.

Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Bw Joseph Kimani alisema kuwa mradi wa kupanda miti ulizinduluwa kirasmi eneo hilo mwaka wa 2019 huku likiwa ni mtindo wa kila mara.

“Tumekuwa tukishirikiana na viwanda tofauti kwa upanzi wa miti,” alisema Bw Kimani.

Afisa wa mazingira katika idara ya majeshi KDF Bi Lisa Gachamba alisema idara hiyo inalenga kupanda miti milioni 50 baada ya miaka kumi.

“Hata hivyo tunalenga kupanda miti milioni moja baada ya mwaka moja ambapo hadi sasa tumepanda miti 150,000,” alifafanua Bi Gachamba.

Alieleza kuwa watazidi kushirikiana na kampuni ya maji ya THIWASCO kuendesha zoezi hilo.

Kampuni ya Thiwasco yapanda miti 1,500 Kang’oki kuvutia nyuni wa angani. PICHA | LAWRENCE ONGARO

Wakati huo pia chuo cha Mount Kenya kiliwakilishwa kwenye zoezi hilo na meneja wa mawasiliano na ushirikiano katika chuo cha Mount Kenya, Bw Boniface Murigi, alipongeza hatua iliyochukuliwa na kampuni ya THIWASCO kwa kushirikiana na washikadau wengine.

“Chuo chetu kimekuwa mstari wa mbele kila mara kushirikiana na kampuni ya maji kupanda miti,” alisema Bw Murigi.

Alisema wanafunzi wa chuo hicho wamekuwa mstari wa mbele kila mara kuona ya kwamba wanajitolea kusaidia katika utekelezaji wa miradi tofauti kote nchini.

Alisema mwanzilishi wa chuo hicho na pia mwenyekiti wa bodi Profesa Simon Gicharu amekuwa katika mstari wa mbele kuendeleza miradi hiyo kupitia wanafunzi.

“Chuo Kikuu cha Mount Kenya kitaendelea kushirikiana na THIWASCO kila mara ambapo wanafunzi wake pia watafuatilia mradi huo ili kuona ya kwamba miti hiyo inanyunyiziwa maji kila mara ili kuzuia isinyauke,” alieleza Bw Murigi.

Alisema wanafunzi wa MKU wanalegenga kupanda miti 20,000 mwaka huu 2023.

  • Tags

You can share this post!

Bajeti kusomwa Juni 15

Empower Smart yabuni apu ya kudhibiti ‘pocket...

T L