• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:00 PM
Kampuni za humu nchini haziruhusiwi kuagiza chanjo – Kagwe

Kampuni za humu nchini haziruhusiwi kuagiza chanjo – Kagwe

Na SAMMY WAWERU

WAZIRI wa Afya Bw Mutahi Kagwe amesema hakuna kampuni ya kibinafsi nchini itakayoruhusiwa kuagiza chanjo ya virusi vya corona kwa sasa.

Bw Kagwe amesisitiza kwamba shughuli hiyo inatekelezwa na serikali pekee.

Waziri ametoa amri hiyo Kenya inaposubiri kupokea dozi ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 wakati wowote kuanzia sasa.

“Kwa sasa serikali ndiyo itashughulikia uagizaji wa chanjo, hakuna kampuni wala mashirika ya kibinafsi yatakayoruhusiwa,” akasema Bw Kagwe.

“Endapo tutafika hapo, watakaopewa idhini sharti wapigwe msasa,” akaeleza waziri. Uingereza na China ni kati ya nchi ambazo zimevumbua chanjo ya janga hili ambalo ni la kimataifa.

Baadhi ya mataifa ulimwenguni yamekumbatia chanjo hizo.

Amri ya Waziri Kagwe kuhusu uagizaji wa chanjo, imejiri wakati ambapo Mamlaka ya Usambazaji Dawa na Vifaa vya Kimatibabu Nchini (KEMSA) imeandamwa na sakata za ufisadi kuhusu utoaji zabuni wa vifaa kuzuia msambao wa virusi vya corona.

You can share this post!

RIZIKI: Mtangazaji wa redio asiyechagua kazi

Mchecheto mitandaoni Karen Nyamu akijaribu kumnasa Samidoh