• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Karen Nyamu atishia kuchochea wanawake Nairobi kuvua nguo kutetea wakazi wa mabanda

Karen Nyamu atishia kuchochea wanawake Nairobi kuvua nguo kutetea wakazi wa mabanda

NA MERCY KOSKEI

Seneta maalum Karen Nyamu ametishia kuwaongoza wanawake wa Kaunti ya Nairobi kuvua nguo katika harakati za kupigania haki na kutambuliwa kwa watu wanaoishi katika mitaa ya mabanda jijini.

Akizungumza wakati wa kikao Bungeni, Nyamu aliunga mkono Mswada uliowasilishwa katika Seneti wa kutetea kuongezwa kwa fedha kwa makazi duni, akisema yanafaa kutajwa kama maeneo yaliyotengwa.

Katika harakati za kutaka Nairobi kufaidika na rasilimali zaidi za mgao, aliapa kuhamasisha wanawake katika kaunti hiyo kuvua nguo barabarani ikihitajika, ili masaibu yao yasikike.

Alisema kuwa kama wakazi wa vitongoji duni wamekuwa wakilia kwa muda mrefu kutokana na kupuuzwa na serikali kwa miaka mingi bila mafanikio.

“Kama wanawake kutoka vijiji vya Laini Saba, Kiboro, Mji wa Huruma…tutavua nguo jijini ikiwa itahitajika ili tusikizwe na hawa watunga sheria wa Bunge hili. Nairobi si kaunti tajiri; Haimanishi sisi ni matajari kwa sababu Nairobi ni makao ya serikali,” alifoka.

Nyamu alinukuu matamshi ya hivi majuzi ya Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti alipokuwa akipigania haki za wakazi wa kaunti yake wakati wa ubomoaji katika ardhi ya kampuni ya East African Portland Cement, akisema ni wakati mwafaka Nairobi kutumia mbinu zozote muhimu kufikisha ujumbe nyumbani.

Kulingana na Nyamu, Nairobi kwa muda mrefu imeachwa nje ya mgao sawa wa bajeti huku ukikisiwa na wabunge wakiitaja Nairobi kama “kaunti tajiri” licha ya takwimu kuonyesha hali tofauti.

“Nairobi imechukuliwa kuwa kaunti tajiri kwa sababu tuna mitaa tajiri kama Karen na Muthaiga, tunawapuuza wakazi wa vitongoji duni wa Nairobi. Nairobi yana makazi ya vitongoji duni kama Kibera, Mathare, Korogocho, Kayabas na Silanga,” alieleza.

  • Tags

You can share this post!

Poleni sana lakini tutapandisha nauli, wamiliki wa matatu...

Viongozi Pwani kufanya kazi na Rais Ruto bila miegemeo ya...

T L