• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 10:50 AM
Kega: Seneta Moi ametosha unga kumrithi Rais Kenyatta

Kega: Seneta Moi ametosha unga kumrithi Rais Kenyatta

Na SAMMY WAWERU

MBUNGE wa Kieni Bw Kanini Kega ameonekana kubadilisha kauli yake ya kumuunga mkono kiongozi wa ODM, Raila Odinga kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao. 

Bw Raila ameashiria kwamba atakuwa debeni 2022, kumrithi Rais Uhuru Kenyatta. Wikendi iliyopita, alifanya ziara maeneo kadha Mlima Kenya katika kile kilionekana kama oparesheni ya kurai jamii ya mlimani kumpa kura.

Bw Kega alikuwa miongoni mwa wabunge na wanasiasa kutoka eneo hilo la Kati chini ya vuguvugu la Kieleweke, walioandamana na Waziri huyo Mkuu wa zamani na kuahidi kumuunga mkono 2022.

Hata hivyo, Alhamisi katika kongamano la KANU ambapo chama hicho kilimteua kiongozi wake, Bw Gedion Moi kupeperusha bendera ya urais uchaguzi mkuu ujao, Kanini alionekana kubadilisha ahadi yake kwa Raila.

“Bw Gedion Moi una vigezo vyote vinavyohitajika kuwa rais mwaka ujao. Ninakuunga mkono,” Kega akasema. Mbunge huyo aidha alisema alipata mwaliko kuhudhuria kongamano hilo la wajumbe wa KANU, kupitia Bw Gedion Moi ambaye pia ni seneta wa Baringo na aliyemtaja kuwa ni “sahibu”.

“Aliponipigia simu, niliwasiliana na bosi wangu ambaye pia ni bosi wenu, Rais Uhuru Kenyatta akanipa ruhusa kuhudhuria,” Bw Kega akadokeza, akihutubia wajumbe.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga, Kalonzo Musyoka (Wiper), Musalia Mudavadi (ANC), Moses Wetangula (Ford-Kenya), na Isaack Ruto (Chama Cha Mashinani) ni kati ya wageni mashuhuri waliohudhuria hafla hiyo.

Kabla ya uchaguzi mkuu wa 2017, KANU ilitia saini mkataba wa makubaliano kushirikiana na chama tawala cha Jubilee. 

  • Tags

You can share this post!

Serikali yawataka wazazi walinde watoto dhidi ya dhuluma na...

KANU yamteua Gedion Moi kuwania urais 2022