• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 6:55 PM
Kimemia alaani ubomozi wa majengo Ol Kalou

Kimemia alaani ubomozi wa majengo Ol Kalou

Na SAMMY WAWERU

Gavana wa Nyandarua Bw Francis Kimemia amekashifu hatua ya Shirika la Reli Nchini (KRC) kutekeleza ubomoaji wa majengo ya wafanyabiashara bila kuwapa muda wa kutosha kujiandaa kuondoa vifaa na bidhaa zao.

KRC imekuwa ikiendeleza ubomozi wa makazi na majengo yaliyo karibu na reli, kwa minajili ya kufufua shughuli za usafiri na uchukuzi kwa njia ya garimoshi kati ya Nairobi, Naivasha, Gilgil, Nyahururu na Nakuru.

Reli hiyo pia inatarajiwa kuelekezwa Kisumu na Malaba.

Mamia na maelfu ya watu wamelalamikia kuathirika, baada ya majengo na bidhaa zao kuharibiwa wakati wa ubomoaji huo.

Eneo la Ol Kalou inakadiriwa zaidi ya watu 3, 000 wameathirika.

“KRC ilipaswa kutoa notisi mapema na kuwapa watu muda wa kutosha wajiandae kuondoka na kuondoa mali yao,” Gavana Kimemia akasema.

Bw Kimemia pia alisema walioathirika wanapaswa kufidiwa, akisisitiza kwamba njia iliyotumika kuwafurusha haikuwa yenye heshima kufuatia uharibifu wa mali yenye thamani ya mamilioni ya pesa.

“Shirika la reli lingetoa mwelekeo ufaao, walioondolewa wafidiwe,” akapendekeza.

Mbali na Ol Kalou, KRC imefanya ubomoaji wa majengo yaliyo karibu na reli eneo la Kisumu, Naivasha, Gilgil na Nakuru ili kuruhusu shughuli za uchukuzi na usafiri kwa njia ya garimoshi kufufuliwa.

  • Tags

You can share this post!

Hofu ya KSSSA kuhusu michezo ya Shule za Upili

Bandari na Ingwe kupigania pointi KPL Ijumaa