• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
Kisura analalamika simtoshelezi chumbani

Kisura analalamika simtoshelezi chumbani

SHANGAZI;

Nina mpenzi lakini kuna jambo linalotishia uhusiano wetu. Kila tukikutana kufurahia mahaba huwa analalamika kuwa simtoshelezi. Nahofia hali hiyo itamfanya aniache. Naomba ushauri wako.

Badala ya kukulaumu mpenzi wako anafaa kukusaidia kurekebisha hali hiyo. Hasa lawama zake zinaweza kuizisha. Anaweza kukusaidia kwa kukuelekeza wakati wa shughuli hiyo ili kuhakikisha anatosheka. Shauriana naye.

Ameshindwa kungoja kuonja tunda, nishauri

Nina miaka 28. Nimekuwa na mpenzi kwa karibu mwaka mmoja. Ndiye mwanamume wa kwanza katika maisha yangu na tulikubaliana ataonja asali tukioana. Sasa anasema hawezi kuvumilia. Nishauri.

Mapenzi ni jambo la hiari, hakuna anayeweza kumlazimisha mwenzake kufanya chochote kile. Kama umeamua utashiriki mapenzi katika ndoa na mpenzi wako ameshindwa kungojea, itabidi mvunje uhusiano wenu.

Ninamlipia mpenzi kodi lakini sijui anakoishi!

Nimekuwa nikigharimia mahitaji yote ya mwanamke mpenzi wangu ikiwemo kodi ya nyumba. Ajabu ni kuwa sijui kwake. Nataka sana kumtembelea lakini nimegundua hataki. Unafikiri ni kwa nini?

Hiyo si kawaida kwa wapenzi hata kama si wewe unayemlipia nyumba. Ni lazima kuna kitu ambacho anakuficha. Huenda ana mpenzi mwingine na ndiyo sababu hataki ujue kwake usije ukawafumania. Chunguza mienendo yake.

Tuliachana na akaoa lakini siku hizi hataki kuniona na mwingine

Nilikuwa nimeolewa lakini nikaachana na mume wangu. Alioa mwanamke mwingine lakini amekuwa akinipigia simu na kunitumia jumbe kuniambia hataki kuniona na mwanamume mwingine. Hiyo ni haki?

Haiwezekani kwa mwanamume huyo kutawala maisha yako ilhali mliachana na akaoa mke mwingine. Anafaa kukusahau na badala yake kuzingatia ndoa yake mpya. Mpuuze, endelee na maisha yako.

>>Usikose safu hii ya Shangazi Akujibu kila Jumatatu hadi Ijumaa 10.30pm -Mhariri

  • Tags

You can share this post!

Wakenya kuhudumiwa matatizo ya afya wakiwa nyumbani, Ruto...

Mahasla sasa kukutana na mkono mrefu wa serikali katika...

T L