• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:15 PM
Wakenya kuhudumiwa matatizo ya afya wakiwa nyumbani, Ruto atangaza

Wakenya kuhudumiwa matatizo ya afya wakiwa nyumbani, Ruto atangaza

NA KEVIN CHERUIYOT

RAIS William Ruto Jumatatu Septemba 25, 2023 alizindua vifaa vya kutoa huduma za kiafya zitakazotolewa kwa wahudumu wa kijamii wa afya (CHP) katika kaunti zote 47.

Akizungumza katika hafla iliyofanyika katika bustani ya Uhuru Park, Rais alisema kwamba wahudumu 100,000 wa kijamii wa afya watakaopokea vifaa hivyo, wanatarajiwa kubadilisha sekta ya afya mashinani, ambapo sasa Wakenya hawatalazimika kuzuru hospitali ili kupokea huduma za kupimwa.

Rais William Ruto wakati wa uzinduzi wa mradi wa kupeleka huduma za afya mashinani. Picha|PCS

“Sasa Wakenya watahudumiwa wakiwa nyumbani na wahudumu hawa ambao watasimamiwa na wafanyakazi wa afya waliofuzu,” alisema Rais Ruto.

Dkt Ruto aliupongeza mpango huu ambao utaendelezwa kwa ushirikiano wa karibu baina ya serikali ya kitaifa na serikali za kaunti.

Kila mhudumu wa afya atahitajika kusimamia nyumba 100 na atapewa vifaa vya kutekeleza vipimo. Aidha, kila mhudumu atapewa simu ya kisasa itakayomsaidia kupokea taarifa muhimu wakati wa kutoa huduma.
Rais Ruto alisema kwamba serikali ya kitaifa na zile za kaunti zitawajibika kwa pamoja kuhakikisha kwamba marupurupu ya wahudumu hawa yanalipwa.

“Kwa kuzindua vifaa muhimu vya wahudumu hawa, ni ishara ya nia yetu ya kuchukua hatua kubwa ya kukabiliana na maradhi, kwa kutumia mtazamo wetu wa bottom up.”

Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu wa Rais Rigathi Gachagua alisema kwamba serikali ya Kenya Kwanza imezindua mpango huu utakaohakikisha kwamba gharama za matibabu kwa Wakenya, zinapunguzwa kwa asilimia 50 katika kipindi cha miaka mitano.

  • Tags

You can share this post!

Kahawa yageuka kuwa chungu kwa Gachagua

Kisura analalamika simtoshelezi chumbani

T L