• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 2:58 PM
Kobia ataka maafisa waadilifu NGEC

Kobia ataka maafisa waadilifu NGEC

Na KNA

WAZIRI wa Utumishi wa Umma, Jinsia, Miradi Maalum na Masuala ya Wazee, Prof Margaret Kobia ametoa wito kwa jopo la watu saba lililoteuliwa kuwapiga msasa wanaosaka kazi ya kuwa Makamishina wa Tume ya Kitaifa ya Usawa wa Jinsia (NGEC) wahakikishe wanaoteuliwa ni watu wenye maadili na waliodhihirisha uongozi bora.

Jopo hilo linalojumuisha Dkt Joyce Nyabuti, Philip Kungu, William Karari, Lucy Karume, Catherine Wameyo, Hedwig Nyalwal na Mary Wairagu litawahoji watu wanaotaka kuzaja nafasi mbili za makamishina zilizoko wazi katika tume hiyo.

Bi Kobia aliwataka saba hao watekeleze majukumu yao kwa makini na waongozwe na katiba pamoja na kanuni za NGEC ili kuwapata watu waliohitimu vyema kujaza nafasi hizo mbili.

Alisema kuwa Wakenya wana matumaini katika utendakazi wa jopo hilo na wanatarajiwa kupata watu wawili wenye ujuzi mkubwa na waliohitimu kutwaa nafasi hizo mbili.

“Niliangalia wasifukazi wa waliounga jopo hili na nikagundua kuwa wote ni watu ambao wamehitimu vizuri katika kazi yao. Natarajia pia watawateua wanaofaa kujaza nafasi hiyo vyema,” akasema Bi Kobia.

Alikuwa akizungumza kwenye hafla ambayo wanachama wa jopo hilo walilishwa kiapo na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NGEC Jacqueline Manani.

Katibu katika Idara ya Utumishi wa Umma Mary Kimonye pia alikuwepo.

You can share this post!

Mumewe mbunge amlaumu Ruto vikali

Are You Able To Be Completamente Genuine Within Online...