• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 5:36 PM
Koome ashangazwa na rundo la kesi 500,000 za wanafamilia wanaopigania mali

Koome ashangazwa na rundo la kesi 500,000 za wanafamilia wanaopigania mali

NA TITUS OMINDE

Nyingi za kesi zaidi ya 500,000 katika vituo mbalimbali vya mahakama nchini, zinahusiana na migogoro ya mali ya familia, Jaji Mkuu Martha Koome amesema.

Akizungumza katika mahakama ya Eldoret siku ya Jumapili, Koome alisikitika kwamba kesi nyingi zinazochangia mrundiko mahakamani zinatokana na mizozo ya mali ya familia.

Koome alitoa wito kwa familia zinazohusika katika mizozo ya mali kukumbatia Mfumo wa Haki Mbadala (AJS) kutatua kesi hizo badala ya kuzirundika katika mahakama kote nchini.

“Kesi nyingi katika mahakama zetu zinahusiana na migogoro ya kifamilia hasa masuala ya ardhi, nashangaa kwa nini familia zinaelekea mahakamani kwa mambo ambayo yanaweza kutatuliwa kirahisi kupitia AJS.”

“Siwezi kuelewa kwa nini kaka na dada au mama na watoto wanapelekana kortini, hata Biblia inatuambia kabla hamjampeleka ndugu mahakamani kwanza tafuteni suluhu kati yenu,” alisema.

Koome alisema mbali na kuchangia mrundiko wa kesi mahakamani, kesi hizo pia zinachangia mfarakano na chuki katika familia. Alikariri kuwa mahakama zinatetea umoja na amani katika familia ndiposa zinahimiza familia kutumia AJS kutatua kesi zao.

Wakati huo huo, alifichua kuwa idara ya mahakama inafanya kazi na Kaunti ya Uasin Gishu kuboresha huduma za mahakama katika eneo hilo kwa kufungua mahakama katika Kaunti Ndogo.

  • Tags

You can share this post!

Ukivurugikiwa na akili, watoto wako nao pia watavurugika...

Wanaharakati: Serikali ya Ruto ilitumia Sh1 bilioni...

T L