• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 9:50 AM
Ukivurugikiwa na akili, watoto wako nao pia watavurugika kitabia -Utafiti

Ukivurugikiwa na akili, watoto wako nao pia watavurugika kitabia -Utafiti

Na CECIL ODONGO

WATAFITI wamebaini kuwa mwanaume akiwa katika hali nzuri ya afya ya kiakili, mtoto ambaye huzaliwa huwa na tabia nzuri na akili wembe.

Utafiti huo uliochapishwa na jarida la Kisaikolojia la Frontiers unaonyesha kuwa si afya ya kiakili tu ya mama huwa na mchango kwenye malezi ya mtoto bali pia hata babake mtoto.

Wakati wa utafiti huo ambao umechukua kipindi kirefu, watoto ambao walikuwa na umri wa miaka sita na zaidi na walikuwa na tabia nzuri. Aidha ilibainika baba wao walikuwa na afya imara ya kiakili wakati ambapo mama walikuwa na ujauzito.

Utathmini wa utafiti huo ulibaini kuwa kuvurugika kwa afya ya kiakili ya mwanaume wakati wa mtoto bado hajazaliwa, huchangia mara mbili kwenye hatari ya kuwa mwehu au kuzaliwa na uwendawazimu.

Malezi ya mtoto anayopewa na babake baada ya kuzaliwa pia huathiri mtoto kitabia hasa wale ambao wana umri wa kati ya miaka sita hadi nane. Iwapo mwanaume atakuwa mlevi au anatumia mihadarati, basi hilo lina uwezo wa kuathiri mdogo huyo kwa kuvuruga tabia zake na pia kiakili.

Mambo mengine ambayo huathiri malezi ya watoto ni migogoro ya mara kwa mara ya familia na kutofautiana kwa wazazi kimawazo kuhusu masuala mbalimbali ya nyumba.

Wanaume wazazi ambao huwapenda watoto wao waliibuka wazazi bora na kama wanaochangia vyema afya ya kiakili ya mtoto.

anaume ambao huwa na watoto wao mara kwa mara na kuwabeba, walibainika husaidia kuwapunguzia watoto hao msongo wa mawazo na kuwapunguzia wao kuishia kuwa na tabia mbovu.

Hata hivyo, watafiti hao walikiri kuwa wanastahili kuzamia zaidi uhusiano ambao upo kati ya mwanaume na mtoto ambaye bado hajazaliwa.

Utafiti huo unastahili kuibuka kwa msingi kuwa mtoto huathirika kiakili na kitabia akiwa na umri wa miaka sita na zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Ushuru: Wafanyabiashara wa Eastleigh watishia kuhamia nchi...

Koome ashangazwa na rundo la kesi 500,000 za wanafamilia...

T L