• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 5:55 AM
Koskei azitaka jamii za Waluo na Wakalenji kuishi kwa amani

Koskei azitaka jamii za Waluo na Wakalenji kuishi kwa amani

NA RUSHDIE OUDIA

MKUU wa Utumishi wa Umma Felix Koskei Jumapili Oktoba 15, 2023 alitoa wito kwa jamii za Waluo na Wakalenjin kuishi kwa amani kwa sababu ni majirani na wana uhusiano ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 1,000.

Akiongea katika eneobunge la Rarieda, Kaunti ya Siaya, Bw Koskei alieleza kuwa jamii hizo ni Waniloti na lugha zao zinafanana na hivyo ni mamoja.

“Jamii za Waluo na Wakalenjin ni majirani na zimefanya biashara ya samaki, mazao ya shambani na maziwa pamoja kwa miaka mingi zaidi.

“Kwa hivyo, hamna haja kwa jamii hizi kutofautiana kwa njia zozote na hata kupigana kwa sababu ni majirani na zimeoana,” akasema katika Kanisa la St Luke Ndara katika eneo la Asembo alipoongoza hafla ya kuchanga peza za kufadhili ujenzi wa Kanisa mpya.

 

  • Tags

You can share this post!

Mudavadi kusaidia kanisa lililoharibiwa paa na upepo Nairobi

Mwanamke Uingereza ajioa mwenyewe baada ya kukosa mume

T L