• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 12:17 PM
Lissu kuzindua kitabu chake leo Nairobi

Lissu kuzindua kitabu chake leo Nairobi

Na JUSTUS OCHIENG

MWANASIASA wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu ambaye amekuwa akiishi uhamishoni nchini Ubeligiji anatarajiwa kuzindua kitabu chake leo jijini Nairobi.

Tundu Lissu aliwasili jijini Nairobi kutoka Ubeligiji Alhamisi.Bw Lissu, mwezi uliopita alifanyiwa operesheni ya upasuaji kutokana na majeraha mabaya aliyopata alipofyatuliwa zaidi ya risasi 20 mnamo Septemba 7, 2017 akiwa jijini Dodoma.

Baada ya kushambuliwa, Lissu alikimbizwa jijini Nairobi ambapo alifanyiwa upasuaji na kisha kuhamishiwa Ubeligiji.Wakili wake Prof George Wajackoya jana alithibitisha kuwa hafla ya uzinduzi huo itafanyika katika hoteli ya Windsor.

Bw Lissu ambaye aliwania urais mwaka jana, alitorokea Ubeligiji baada ya uchaguzi mkuu akidai kuwa maisha yake yalikuwa hatarini.“Rais Samia Suluhu anafaa kunieleza mimi, Watanzania na ulimwengu mtu aliyenipiga risasi. Waliamrishwa na nani? Ukimya wake unatia wasiwasi,” akasema Bw Lissu kupitia mtandao wa Twitter mnamo June 8, mwaka huu.

Baada ya hafla ya uzinduzi Bw Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ataelekea jijini Dar es salaam ambapo atakuwa mmoja wa wazungumzaji wakati wa maadhimisho ya Siku ya Katiba, Julai 1, 2022.

Katika kitabu chake, Bw Lissu anaelezea mageuzi ya mabunge ya Afrika Mashariki; Kenya, Tanzania na Uganda.Bw Lissu anasema kuwa mabunge ya Afrika Mashariki ni vibaraka wa watawala na hakuna tofauti na enzi za ukoloni.

“Mabunge ya Afrika Mashariki, isipokuwa Kenya, hayana uhuru kwani yanaendeshwa na marais walio mamlakani,” anasema Bw Lissu.

  • Tags

You can share this post!

Raia wakatae siasa chafu za uhasama

Wazazi wapewa tahadhari kuhusu mkurupuko wa nimonia