• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 9:55 AM
Madaktari bandia washtakiwa kudunga watu chanjo bandia ya Johnson & Johnson

Madaktari bandia washtakiwa kudunga watu chanjo bandia ya Johnson & Johnson

Na RICHARD MUNGUTI

MADAKTARI wawili bandia walishtakiwa jana kwa kuwadunga watu chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 wakidai ni ile ya Johnson & Johnson.

Mabw Wallace Mugendi Njiru na  Kenneth Mukundi Njeru walikabiliwa na mashtaka matano ya kupokea zaidi ya Sh200,000 kutoka kwa watu waliodungwa chanjo hiyo kati ya Agosti 10-13, 2021.

Kwa jumla washukiwa hao walikabiliwa na mashtakiwa 11 ya kujifanya wao ni madaktari kutoka hospitali kuu ya Kenyatta (KNH), kughushi vitambulisho vya  KNH, kughushi leseni za baraza la kuwasajili madaktari , kughushi leseni ya hospitali ya kibinafsi na kupokea pesa kwa njia ya udanganyifu.

Njiru na Njeru walishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bi Martha Nanzushi.Washtakiwa hao walikabiliwa na shtaka la kujifanya kuwa madaktari kutoka hospitali ya KNH kati ya  Julai 24 2017 na Septemba 7,2021 katika eneo la Roysambu Kasarani kaunti ya Nairobi.

Shtaka hilo lilisema katika kipindi hicho cha miaka minne wamekuwa wakiwatibu watu katika hospitali ya kibinafsi ya  Crane Hospital.Washtakiwa hao walikabiliwa na shtaka lingine la kughushi kitambulisho cha Daktari cha KNH wakidai walikuwa wameajiriwa na hospitali hii kuu na kubwa zaidi katika eneo la Afrika mashariki.

Pia walishtakiwa kughushi leseni nambari 00944 wakidai imesajiliwa na baraza la kitaifa la madaktari KMPDC.Wawili hao hawakuwakilishwa na wakili.Waliomba waachiliwe kwa dhamana.

Upande wa mashtaka ulioongozwa na Bi Everlyn Onunga haukupinga washtakiwa wakiachiliwa kwa dhamana.Kesi dhidi yao itatajwa baada ya wiki mbili kwa maagizo zaidi

  • Tags

You can share this post!

Everton wapepeta Burnley na kutinga nne-bora EPL

Mourinho raha tupu baada ya kushinda mechi yake ya 1,000...