• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 5:30 PM
Mahasla wafunga biashara kupisha Mfalme Charles III kuingia Fort Jesus

Mahasla wafunga biashara kupisha Mfalme Charles III kuingia Fort Jesus

NA CHARLES ONGADI

Wauzaji madafu, tende, achari, viazi karai, juisi, na akina mama wauzaji vyakula katika barabara inayoelekea Fort Jesus, walikosa kufungua biashara zao kama kawaida baada ya kupokea habari ya ziara ya mfalme Charles na mkewe Camilla.
Tsuma Ndegwa anayeuza madafu kandokando ya barabara ielekayo Fort Jesus anasema alifunga biashara yake jana Alhamisi baada ya kupokea habari ya ziara hiyo.
“Sikutaka kutatizwa na maaskari wa Kaunti ya Mombasa wala maafisa wa kiusalama nikaamua kutofanya kazi Alhamisi, ” akasema Ndegwa.
Hali ilikuwa hivyo kwa Bi Amina Kazungu ambaye ni muuzaji wa vyakula karibu na lango la Fort Jesus aliyeiambia Taifa Leo kwamba hakuweza kufungua biashara yake leo kupisha ziara hiyo.
Aidha, kulingana na Bw Abdallah Said anayeuza juisi eneo hilo anasema ataanza tena biashara yake siku ya Jumamosi mara baada ya pilkapilka za kumkaribisha mfalme huyo zitakapomalizika.
Katika maeneo mengine ya jiji la Mombasa, baadhi ya wauzaji wa biadhaa kandokando mwa barabara ielekayo kivuko cha Likoni,walionekana wakifunga biashara zao kwa hofu ya kutatizwa na maaskari wa Kaunti ya Mombasa walioonekana kwenye malori yao wakivinjari.
Lakini wenye biashara ya uchukuzi wa Tuk Tuk waliendelea kufanya biashara zao pasina usumbufu.
  • Tags

You can share this post!

Yafichuka visa vya wizi wa magurudumu ya magari huongezeka...

Masaibu ya chokoraa wa kike wasiopata huduma za upangaji...

T L