• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Maktaba ya kitaifa kurejelea huduma zake za kitaifa kwa umma

Maktaba ya kitaifa kurejelea huduma zake za kitaifa kwa umma

Na CHARLES WASONGA

WAKENYA sasa wataruhusiwa kupata huduma za kawaida katika maktaba za umma kuanzia Jumatatu, Februari 1, 2020.

Hii ni baada ya matawi 64 yote ya Maktaba ya Kitaifa Nchini (KNLS) kufungwa baada ya mlipuko wa Covid-19 nchini kuanzia Machi 13, 2020.

Katika ujumbe kupitia akaunti yake ya twitter na tangazo lililolipiwa magazetini, KNLS ilisema matawi yake yote yataanza kutoa huduma kwa za kawaida kwa umma huku akizingatia masharti yote ya kuzuia msambao wa ugonjwa huo hatari.

Saa za huduma zitasalia kuwa kati ya saa mbili za asubuhi (8.00 am) hadi saa kumi na mbili na nusu jioni (6.30 pm) kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Siku za Jumamosi maktaba hizo zitafunguliwa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi (8.30 am) hadi saa kumi na moja jioni (5.00pm).

Hata hivyo, matawi yote 67 ya KNLS yatasalia kufungwa siku za Jumapili na sikukuu za umma.

“Watumiaji huduma za maktaba wanahimizwa kuzingatia kanuni za kuzuia kuenea kwa corona kwani vifaa hitajika vimetolewa,” ikasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo pia iliongeza kuwa makao makuu ya KNLS imehamishwa hadi jumba la Maktaba Kuu, lililoko eneo la Community, Nairobi kutoka majengo ya tawi la maktaba ya kitaifa la mtaa wa Buruburu.

Kenya imeendelea kuandikisha idadi ndogo ya visa vya maambukizi ya corona tangu Desemba 2020 hali ambayo imesababisha shughuli nyingi kuanza kurejelea hali ya kawaida.

Shule zimefunguliwa kwa masomo ya kawaida kuanzia Januari 4, 2021, na mitihani ya kitaifa ya darasa la nane (KCPE) na Kidato cha Nne (KCSE) imeratibiwa kuanza mwezi Machi 2021.

Hata hivyo, Wizara ya Afya ingali inasisitiza kuwa Wakenya wanafaa kuendelea kuzingatia masharti ya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

  • Tags

You can share this post!

Benchi ya kiufundi ya Kenya Morans sasa yajivunia maarifa...

Afunguka kueleza jinsi anavyoishi baada ya kutemwa