• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Mama asimulia jinsi mpenziwe alivyoua mtoto kinyama

Mama asimulia jinsi mpenziwe alivyoua mtoto kinyama

NA JOSEPH OPENDA

MWANAMKE mmoja amesimulia Mahakama Kuu ya Nakuru jinsi mwanaume aliyekutana naye kama mpenzi alimuua mwanawe, aliyemchukulia kuwa kikwazo kwa mapenzi yao.

Bi Eunice Wangui alisimulia korti jinsi Daniel Obonyo alimuua mwanawe wa kike kwa kumgonga na kifaa butu kichwani.

Mshtakiwa aliyekuwa amesafiri nyumbani kwao Kisii, alimpigia simu Bi Wangui na kukiri kumuua bintiye Gabriella Mellisa, aliyeaga dunia katika Hospitali Kuu ya Nakuru.

Ripoti ya upasuaji iliashiria mtoto huyo aligongwa na kifaa butu kichwani na kufuta fikira za awali kuwa alikuwa amenyongwa na chakula jinsi ilivyokuwa imedaiwa.

Wapasuaji pia walisema mtoto alikuwa na uvimbe wa damu kwenye ubongo wake.

Madaktari wasiopungua wanne waliokuwa wamemhudumia mtoto huyo awali hawakutoa jibu lolote kuhusu shida ya mtoto huyo.
Mmoja wao alimweleza Bi Wangui kuwa mtoto wake ana anemia lakini akakataa kwa sababu alifahamu mtoto wake alikuwa anaugua kisukari.

Yote yalianza Bi Wangui alipotembelewa na mpenziwe nyumbani kwake katika eneo la JB, Nakuru mnamo Oktoba 17, 2018.

Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Samuel Mohochi, mama huyo alisimulia jinsi ziara ya Obonyo ilivyomjaza hofu mtoto wake aliyeanza kulia kwa nguvu, ishara ya kwanza ya hatari aliyoipuuza.

Bi Wangui alikuwa nyumbani kwa jirani yake pamoja na mtoto wake wakati huo.

“Alienda moja kwa moja hadi alipokuwepo mtoto na akamchukua. Mtoto alianza kupiga mayowe lakini Obonyo akapuuza kilio chake na kumbeba,” alieleza Bi Wangui.

Mama huyo alikwenda nyumbani kwa dada yake na kumwomba akae na mtoto wake kwa muda ili aweze kuwa na wakati na Obonyo.
Dada yake, hata hivyo, alikataa akidai alikuwa na ushirika wa kanisa siku hiyo.

Obonyo alidai kuhisi njaa na akampa Wangui Sh150 kwenda kununua chakula ambapo mama huyo alimwacha bintiye na mpeziwe kabla ya kuelekea sokoni.

Aliporejea baada ya dakika 20, Bi Wangui alimpata mtoto wake akilia sana kabla ya kumchukua na kumnyonyesha.

“Niligundua kichwa cha mtoto kilikuwa na mchanga kwenye upande mmoja lakini nilipomuuliza akasema alimweka chini kumaanisha huenda aliutoa chini.”

Mwendo wa saa 12 jioni, Bi Wangui alimwalika Obonyo kujiunga naye kwenda ushirika lakini akakataa na kusema angebaki nyumbani na mtoto.

Akiwa huko alimtuma dada yake mdogo kuchukua chai na vikombe ambapo alirudi dakika chache baadaye akiwa amejawa na hofu na kumweleza amempata Obonyo akiwa amemshika mtoto nje ya nyumba.”

“Aliniambia mtoto alitoa sauti iliyomtishia alipokuwa akimlisha akadhani amenyongwa. Nilijaribu kumfanyia huduma ya kwanza na kuabiri gari kuelekea hospitali ya Mirugi Kariuki.”

Mwanamke huyo pia alisimulia wakati Obonyo alimpa simu yake ambapo alikuta picha na video alizochukua za mtoto wake akilia kabla ya kufa.

“Niliona video nyingine iliyorekodiwa ikimwonyesha Obonyo na mtoto wangu usiku akijaribu kufungua macho yake kwa kutumia vidole vyake. Kwenye video hiyo niliona macho ya mtoto wangu yalikuwa mekundu.”

  • Tags

You can share this post!

Aliyevuruga mkutano wa Ruto atozwa faini ya Sh13,000

Nike yamjengea Kipchoge sanamu ya shaba Amerika

T L