• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 2:35 PM
‘Mapasta’ wahuni wasukumwa jela miaka 151 kwa ubakaji

‘Mapasta’ wahuni wasukumwa jela miaka 151 kwa ubakaji

NA RICHARD MUNGUTI

WAHUBIRI wawili wamehukumiwa kifungo cha idadi jumla ya miaka 151 jela kwa kuwadhulumu kimapenzi watoto wa umri mdogo.

Mapasta hao ni mmishenari kutoka Ujerumani na pasta wa Kipendekosti.

Wawili hao, Thomas Scheller (Mjerumani) alifungwa miaka 81, naye James Njugunga Kuria alisukumwa kula maharage miaka 70.

Scheller atatoka jela akiwa na umri wa miaka 155, mwaka wa 2104,

Walishtakiwa kutenda uhalifu huo katika maeneo ya Nyalenda – Kisumu na Ngong, Kaunti ya Kajiado ambapo walikuwa wamejenga makanisa kuhudumia wakazi.

Scheller, 74, aliyestaafu kazi ya Uhandisi na kuja Kenya kama Mmishenari, alifululiza hadi kaunti za Kisumu, Kilifi na Nairobi ambapo aliwadhulumu kimapenzi wavulana wa umri kati ya miaka 10 na 13.

Mshtakiwa alitiwa nguvuni mnamo Mei 2020, akijaribu kutoroka nchini Kenya.

Mbali na kuwadhulumu kimapenzi, Scheller alikuwa anapiga picha za watoto wakishiriki ngono na kuzipeperusha mitandaoni kwa wandani wake katika biashara hiyo chafu.

Kuria aliomba msamaha akisema anaugua maradhi ya akili na “anstahili kupelekwa hospitali badala ya kufungwa jela.”

  • Tags

You can share this post!

Jinsi manukato ya udi yanavyovutia wateja kununua bidhaa 001

Bei ya lishe ya mifugo kushuka

T L