• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 7:50 AM
Matokeo ya somo la Kiswahili yaimarika pakubwa

Matokeo ya somo la Kiswahili yaimarika pakubwa

Na LEONARD ONYANGO

WATAHINIWA walifanya vyema katika somo la Kiswahili kwenye Mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) wa mwaka huu ikilinganishwa na 2019.

Matokeo yaliyotangazwa jana yanaonyesha kuwan matokeo ya somo la Kiswahili yaliimarika katika mtihani wa mwaka huu licha ya watahiniwa kuwa nyumbani kwa muda mrefu kutokana na janga la virusi vya corona.

Kulingana na Profesa Magoha, watahiniwa pia walifanya vyema zaidi katika masomo ya insha ya Kiingereza, Lugha ya Ishara, Hisabati na Somo la Dini ikilinganishwa na 2019.

Hata hivyo, matokeo ya Insha ya Kiswahili yalidorora ikilinganishwa na 2019.

Masomo mengine ambayo matokeo yake yalidorora ikilinganishwa na 2019 ni Kiingereza, Sayansi na Somo la Jamii.

Chris Gatatha aliyepata alama 406 kwa KCPE ashangiliwa kwa kuiletea faraja Shule ya Msingi Pink Roses, Githunguri, Kaunti ya Kiambu. Picha/ Hisani

UFADHILI WA KARO

Watahiniwa wa kike walifanya vyema katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Lugha ya Ishara ilhali wenzao wa kiume waling’aa katika masomo ya Hisabati, Sayansi, Somo la Jamii na Somo la Dini.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoga alisema wanafunzi 9,000 kutoka familia zisizojiweza kimapato watapewa ufadhili wa masomo na serikali chini ya Mpango wa Ufadhiliwa Elimu.

Waziri Magoha alisema wizara ya Elimu imeanza kujiandaa kwa ajili ya Mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) na Kidato cha Nne (KCSE) wa mwaka ujao huu.

You can share this post!

Mabinti wabwaga wavulana

Mwanachuo akana kuua familia yake