• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 11:02 AM
Messi aisaidia Argentina kufuzu kwa robo fainali kipute cha Copa America

Messi aisaidia Argentina kufuzu kwa robo fainali kipute cha Copa America

BRASILIA, Brazil

ARGENTINA imefuzu kwa robo-fainali ya michuano ya Copa America baada ya kuishinda Paraguay kwa 1-0, lililofungwa na Alejandro Gomez baada ya kuandaliwa pasi na Angel Di Maria, ugani Estadio Nacional Mane Garrincha.

Hii ilikiwa mara ya 147 kwa Messi kuchezea timu hiyo ya taifa, ambapo sasa amefikia rekodi ya kiungo mstaafu Javier Mascherano. Ulikuwa ushindi wa pili mfululizo kwa timu hiyo katika mashindano haya ya mataifa ya Amerika Kusini, ikiwa mara ya 16 kwa timu hiyo kutoshindwa tangu wabanduliwe katika nusu-fainali ya michuano hiyo mnamo 2019.

Matokeo hayo yameiweka Argentina kileleni mwa Kundi A baada ya kujikusanyia jumla ya pointi saba kutokana na mechi tatu, pointi mbili mbele ya Chile, na nne mbele ya Paraguay na kisha mbele ya Uruguay.

Bolivia wanashikilia nafasi ya mwisho kundini humo bila chochote.Kwingineko, Arturo Vidal alifunga langoni mwake na kuipa Uruguay bao la kwanza kabla ya kuagana 1-1 na Chile iliyopata bao la kusawazisha kupitia kwa Eduardo Vargas, dakika ya 26.Matokeo ya mechi za Jumatatu usiku ni: Venezuela 2 Ecuador 2, Colombia 1 Peru 2.

  • Tags

You can share this post!

Papara na pupa hazileti ufanisi katika maisha

Covid-19: WHO sasa kuzindua kituo chakuunda chanjo Afrika