• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 1:12 PM
Covid-19: WHO sasa kuzindua kituo chakuunda chanjo Afrika

Covid-19: WHO sasa kuzindua kituo chakuunda chanjo Afrika

Na MHARIRI

JUHUDI za kukabiliana na Covid-19 huenda zikapigwa jeki pakubwa huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likianzisha kituo cha mafunzo kuhusu chanjo za Covid-19 na utoaji leseni kwa kampuni kutoka mataifa maskini.

WHO ilisema Jumatatu kuwa itaanzisha kituo hicho nchini Afrika Kusini, hatua ambayo Rais Cyril Ramaphosa aliitaja kama ya kihistoria katika usambazaji wa teknolojia hiyo ya kuokoa maisha.

“Kituo cha “kuhamisha teknolojia” huenda kikawezesha nchi za Kiafrika kuanza kuunda chanjo za mRNA – ambayo ni teknolojia ya hali ya juu inayotumika kwa chanjo kutoka kampuni za Pfizer-BioNTech na Moderna – katika muda wa miezi 12 pekee,” alisema WHO.

Tangazo hilo lilitolewa na Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa chanjo kote Afrika, ambapo maambukizi na vifo kutokana na virusi vya corona, viliongezeka kwa takriban asilimia 40 katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

“Hii leo nina furaha kutangaza kuwa WHO inajadiliana na kampuni na taasisi mbalimbali ili kuanzisha kituo cha kuhamisha teknolojia Afrika Kusini,” “Shirika hilo linajumuisha kampuni ya Afrigen Biologics & Vaccines, ambayo itatumika kama kituo cha kuunda chanjo za mRNA na kutoa mafunzo kwa kiwanda cha Biovac,” alisema Tedros. kupitia taarifa jijini Geneva.

  • Tags

You can share this post!

Messi aisaidia Argentina kufuzu kwa robo fainali kipute cha...

Washukiwa 15 wa mauaji kuendelea kusota rumande