• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 11:39 AM
Mjadala mkali wa mapadri kuendelea kuzimwa kuoa

Mjadala mkali wa mapadri kuendelea kuzimwa kuoa

NA MWANGI MUIRURI

MAPADRI wa kiume, kwenye muungano uliolegeza msimamo wa Kanisa wa kuwazima kuoa, wamesema wakati umefika wa kuangazia changamoto inayowakabili baadhi yao kuhusu hisia za kimwili.

“Mambo mengi ya aibu yanawakuta mapadri? Kuna baadhi wameaga dunia huku wengine wakiwekewa mchele kwa vinywaji ndani ya mikahawa. Kwa kweli wengi wanalemewa na hisia za kimwili,” akasema mshirikishi wa kampeni hizo Dikoni Edwin Wagura.

Bw Waiguru alisema kwamba “si jambo la busara kukaa katika mtazamo potovu wa kuumiza binadamu kwa itikadi ambazo hata hazieleweki ziliundiwa wapi”.

Akasema: “Tukizusha, tunaambiwa ikiwa tunaona ugumu wa kukaa bila ngono tuende tu tuoe”.

Bw Wagura anashikilia kuwa Mungu alisema “si vyema mwanamume kuishi peke yake”.

“Cha msingi ni kwamba, huu ukatili wa kuzima mwanamume aliye sawasawa kihisia uhuru wa kushiriki ngono unafaa kuondolewa hata ikiwa ni kupitia maandamano au kesi mahakamani,” akasema.

Bw Wagura alisema kwamba “visa vya aibu vinavyohusu mapadri havijengi kanisa ama injili”.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Presha kwa Mandago awaambie wazazi, wanafunzi alikopeleka...

Azimio wazindua vuguvugu la ‘Tumechoka Citizens’

T L