• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Mkuu wa polisi Makadara athibitisha maafisa wa DCI wanachunguza kifo tata cha mfanyakazi wa benki

Mkuu wa polisi Makadara athibitisha maafisa wa DCI wanachunguza kifo tata cha mfanyakazi wa benki

NA SAMMY KIMATU

WAPELELEZI katika kituo cha polisi cha Industrial Area wameanzisha uchunguzi rasmi kuhusu kisa cha mfanyakazi wa benki aliyeripotiwa kutoweka na kisha mwili wake kupatikana katika nyumba yake.

Mkuu wa polisi katika eneo la Makadara Bi Judith Nyongesa alisema Mercy Gacheri Kaburu,35, hakuripoti kazini katika benki ya ABC, Tawi la Westlands.

Aliongeza kwamba mwili wake ulikuwa nusu uchi akiwa kitandani huku sindano mbili zilizotumiwa zikiwa kando ya mwili wake.

Miguu yake ilikuwa imegusa sakafu ehuku damu ikimtoka mdomoni mwake.

Maskani yake yalikuwa Podium Apartments katika lokesheni ndogo ya Balozi, tarafa ya South B, kaunti ndogo ya Starehe.

Bi Nyongesa aliongeza kwamba iliwalazimu maafisa wake kutafuta huduma za fundi wa kuchomelea vyuma ndiposa wakapata nafasi ya kuingia ndani ya nyumba baada ya kuvunja mlango.

Baada ya mwenzake mmoja kazini kudokezea polisi habari kuhusu kupotea kwake tangu wiki jana huku juhudi za watu kumpigia simu bila kujibiwa kuwatia wengi wasiwasi ndiposa akaanza kutafutwa.

Mwili wake ulipatikana Alhamisi jioni baada ya wafanyakazi wenzake kumtembelea nyumbani kwake.

Wenzake walisema alikaa peke yake na walikuwa na wasiwasi kuwa hakujibu simu zao wala jumbe fupi.

Akiongea na Taifa Leo, naibu kinara wa upelelezi wa uhalifu wa Jinai eneo la Makadara, Bw Jared Seko alisema wameanzisha uchuguzi kuhusu tukio hilo.

Aidha, haijulikani kama alikuwa mgonjwa.

“Sindano mbili zilizotumika zilipatikana kando ya mwili wake ukiwa nusu uchi, damu ikitoka mdomoni mwake,” Bi Nyongesa akasema.

Mwanamke huyo alifanya kazi kama afisa wa fedha.

Mwili huo ulipatikana ukiwa juu ya kitanda huku kichwa kikitazama kando nayo miguu ikigusa sakafu.

Mikono yake miwili ilikuwa na alama za kudungwa kwa sindano.

Hata hivyo, damu ilikuwa ikitoka mdomoni, polisi walisema.

Mwili wake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City.

Kwingineko, mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 55 ulipatikana kando ya barabara katika mtaa wa Kibera.

Haijabainika ni nini kilichosababisha kifo chake.

Polisi walisema mwili wake ulipatikana Alhamisi jioni na wapita njia ambao walimfahamu.

Watembeao kwa miguu walimjulisha mmiliki wa nyumba marehemu alikokodi ambaye alipigia polisi simu.
Polisi waliuchukua mwili huo na kupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti wakisubiri upasuaji.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamke ashtakiwa kuishi na jambazi na kukosa kuarifu...

Viongozi Mlimani lawamani kwa ‘kuwa waoga’...

T L