• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:44 PM
Mudavadi na Wetangula watakiwa kuvunja vyama vyao wajiunge na UDA

Mudavadi na Wetangula watakiwa kuvunja vyama vyao wajiunge na UDA

NA JESSE CHENGE 

KATIBU Mkuu wa Chama cha United Democratic Alliance (UDA), Cleophas Malala, pamoja na viongozi wengine kutoka Bungoma, wamehimiza viongozi wa Muungano wa Kenya Kwanza kuvunja vyama vyao na kujiunga na UDA kwa ajili ya umoja na maendeleo ya Magharibi mwa Kenya.

Kulingana na Malala, kuwepo kwenye muungano mmoja kama jamii, eneo hilo litanufaika kimaendeleo na serikali ya sasa.

Bw Malala pia anasema ni kutokana na umoja wa jamii ya Magharibi, itapata kiongozi mwenye ushawishi mkubwa.

“Tunahitaji kiongozi mwenye nguvu kutoka jamii ya Luhya na tunapaswa kuvunja vyama tujiunge na UDA,” alisema Bw Malala.

Malala anasema UDA ina uwezo kuunganisha nguvu za viongozi bila migogoro ya kisiasa.

Katibu mkuu huyo wa chama tawala kinachoongozwa na Rais William Ruto, alitoa matamshi hayo mnamo Jumapili, Septemba 24, 2023 alipoungana na viongozi wengine wa Magharibi mwa Kenya, eneo la Mlima Elgon kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa.

Viongozi waliohudhuria hafla hiyo walitoa wito kwa Mkuu wa Mawaziri, Musalia Mudavadi (ANC) na Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetangula (Ford-Kenya) kuungana nao na kuvunja vyama vyao, wakiwahimiza kujiunga na UDA.

“Chama cha UDA kinatoa fursa ya kuunganisha nguvu zetu na kutoa mwelekeo wa kisiasa bila migogoro,” Malala akasisitiza.

Hata hivyo, walikosoa Kamati ya Wabunge wa Mkoa wa Magharibi kwa kujihusisha na siasa za uchaguzi wa 2032 badala ya kutekeleza mipango ya serikali kwa ajili ya maendeleo ya eneo hilo.

Aidha, wanasiasa hao walizindua kampeni kuwashawishi wafuasi wa vyama vingine kujiunga na UDA.

 

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Wazee wampa kijana marufuku ya muda kwa kunywa pombe kabla...

Gavana Kawira roho mkononi UDA ikiunga mkono abanduliwe

T L